June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DCB yazindua ‘huduma kwa mteja’

Spread the love

BENKI ya DCB leo imezindua wiki ya huduma kwa wateja wake ikiwa ni moja ya hatu za kuonesha inawatambuwa, kuwashukuru na kuwajali. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Haika Machaku amesema wanajivunia kuwa sehemu ya maendeleo ya wateja wao kutokana na mikopo waliyoanza kuitoa tangu mwaka 2008 iliyowezesha wananchi kununua viwanja na kujenga nyumba.

Machaku amesema kauli mbiu ya benki hiyo kwa mwaka huu ni ‘Tupo kwa ajili yenu’ ambayo inadhihilisha lengo lao juu ya utoaji wa huduma bora zenye staha na kukidhi matakwa ya wananchi.
Amesema katika kuhakikisha huduma bora kulingana na mahitaji ya wateja wao, wameweka njia nyingi za mawasiliano yaliyowezesha kupokea maoni kutoka kwa wateja.

“Pamoja na kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja ya mwaka huu pia tumeboresha huduma ya mikopo kwa wateja wetu. Kwa sasa wanaweza kupata mikopo ya nyumba kwa gharama nafuu sana,” amesema Machaku.

Mmoja wa wateja wa benki ya DCB, Mwajuma Kombo amesema huduma za benki hiyo ni nzuri na zinawasaidia katika kutatua mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kujenga nyumba na kununua nyumba pia kupitia mikopo inayotolewa.

Kombo amewashukuru watendaji wa benki hiyo kwa kuanzisha wiki hiyo ya huduma kwa wateja kwani inaonyesha ikuwa benki hiyo inawajari wateja wake.

“Nimejiunga na benki ya DCB tangu ilipoanza kutoa mikopo mwaka 2008 hadi sasa na mambo mengi nimeweza kuyafanya kupitia mikopo hiyo ikiwemo kusomesha watoto na kujenga nyumba yangu mwenyewe.” amesema Kombo.

error: Content is protected !!