September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DC Utaly: ‘kitanzi’ kwa wafugaji wabishi kipo tayari

Mifugo ikichungwa

Spread the love

SERIKALI wilayani Mvomero, Morogoro imezindua zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo ikiwa ni pamoja na kupiga chapa mifugo yote halali kulingana na ukubwa wa eneo huku ikiahidi kutoza faini wafugaji watakaozuia zoezi hilo, anaandika Christina Haule.

Mohamed Utaly, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, amesema kuwa wafugaji watakaobainika kuzuia zoezi hilo la serikali watatozwa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000/=) au kifungo jela.

DC huyo alikuwa akizungumza na viongozi wa wafugaji, maafisa mifugo wa kata zote, watendaji na viongozi wa mashirika na mitandao ya wafugaji.

“Wapo watu wanataka kutengeneza mgogoro kati ya Serikali na wafugaji kwa manufaa yao ili serikali ionekane inafanya zoezi hili kwa lengo la kuichukua mifugo ya wafugaji jambo ambalo si la kweli,” amesema DC Utaly.

Florent Kayombo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Mvomero, amesema upigwaji wa chapa katika ng’ombe hao ni utekelezaji kwa kanuni za kimataifa ili wafugaji waweze kuzalisha nyama inayokubalika katika masoko ya kimataifa.

Ngirimo Sangaini, mfugaji kutoka Kijiji cha Lukenge, ameeleza kushangazwa na kitendo cha serikali kutoa taarifa hiyo ya utekelezaji badala ya kuanza kutoa elimu kwanza, kitu ambacho kinaweza kusababisha wafugaji wenzake wakagomea zoezi hilo.

error: Content is protected !!