Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko DC Nyamongo: Jiungeni CHF ili mnufaike
Habari Mchanganyiko

DC Nyamongo: Jiungeni CHF ili mnufaike

Spread the love

VUMILIA Nyamoga, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, amewataka watendaji wa wilaya hiyo kutoa elimu ili wananchi waweze kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Anaripoti Dandosn Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Augost1 2019, akizungumza na madiwani na watendaji wa idara mbalimbali kwenye kikao cha baraza la madiwani cha utekelezaji kwa kipindi cha cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Amesema, watendaji wakihakikishe kuwa wanatoa elimu kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha na kujiandikisha ili waweze kuapata huduma pale wanapopatwa na matatizo.

Vumilia amesema, wananchi kama watajiandikisha kwa wingi, itasaidia kuondoa malalamiko ya kuwa hawapati huduma au kutibiwa kwa gharama kubwa.

“Wakishiriki kikamilifu itaondoa malalamiko ya kutopata huduma hiyo ya mfuko wa afya ya jamii ambayo ilimeboreshwa,” amesema.

Athumani Masasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia vyanzo vya mapato ikiwemo na miradi ili pato la uchumi liweza kuongezeka.

Amesema, ili halmashauri hiyo iweze kuongezeka kiuchumi, watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia na kukamilika kwa miradi yote ili iweze kuhudumia wananchi kwa ajili ya maendeleo.

“Ninawaomba madiwani pamoja na watendaji hakikisheni mnasimamia miradi ili halmashauri yetu, mapato yake yaweze kuongezeka kwa kupitia vyanzo hivyo vya miradi,”amesema.

Samweli Kaweya, mwenyekiti wa halmashauri hiyo wamewataka watumishi kuwa na ushirikiano ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa ajili ya maendeleo yao.

Na kwamba, ushirikiano huo ukiwepo halmashauri itakuwa imefanikiwa kwenye maenedeleo yake ya kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!