July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mwanza ambeza Kikwete, ajipendekeza kwa Magufuli

Spread the love

MAGESA Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (DC) anajipendekeza kwa Rais John Magufuli huku akimbeza Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. Anaandika Moses Mseti.

Mulongo amesema, wakati wa uongozi wa Rais Kikwete ambaye amemaliza uongozi wake tarehe Desemba mwaka jana, vyombo vya dola hususan mahakama havikuwa huru na kusababisha wananchi wengi kuona havina msaada kwao.

DC huyo ambaye ni mteule wa Rais Kikwete, amesema hayo ikiwa takribani ni miezi mitatu baada ya Rais Magufuli kushika madaraka ya kuongoza Tanzania.

Mulugo ametoa kauli hiyo wakati wa kilele cha Siku ya Sheria Tanzania, kilichofanyika katika Ofisi za Mahakama ya Mkoa wa Mwanza zilizopo katika eneo la Kamanga, Kata ya Nyamagana.

Kiongozi huyo amedai kuwa, kwenye utawala wa Rais Kikwete wananchi walikuwa wakiogopa kwenda mahakamani kudai haki lakini sasa ni tofauti a kuwa chombo hiko kimeimarika.

Kwenye kilele hicho amesema amedai kuwa wananchi wanapaswa kutambua kwamba, hivi sasa mahakama hazina mchezo wala muda wa kumbeba mtu yeyote hata kama ni kiongozi wa serikali.

Hata hivyo amedai wakati uliopita wananchi walikuwa wakishindwa kupeleka kesi za madai yao mahakamani wakihofia kuminywa kwa haki zao lakini hivi sasa mambo yote yapo wazi.

“Watu wengi wanapoteza haki zao kwa kushindwa kufika mahakamani na wameshindwa kufahamu kwamba sasa hivi hata jambazi akiona polisi anamsumbua anataka apelekwe haraka mahakamani ili kutolewa utatuzi,” amesema Mulongo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Vicent Makalamba amesema kuwa, wajibu wao ni kutoa haki kwa wananchi.

error: Content is protected !!