June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mulongo awekwa kiti moto

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

Spread the love

MADIWANI wa Manispaa ya Ilemela jijini hapa, wamemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kutoa majibu ya kina juu ya kushindwa kwenda safari ya kujifunza namna bora ya upangaji wa jiji hilo. Anaandika Moses Mseti … (endelea). 

Madiwani hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walitoa kauli hiyo wakati Mkurugezi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga akiwasilisha taarifa ya ziara ya mafunzo yaliyofanyika mjini Dubai.

Hata hivyo, madiwani hao wamesema kitendo cha Mulongo kushindwa kuwasili katika ziara hiyo kimesababisha wananchi kushindwa kuwa na imani na viongozi wao hivyo ni vyema akawaeleza sababu za kushindwa kushirikiana na viongozi wenzake.

Mmoja wa viongozi hao ambaye hakuwa tayari jina lake kuandikwa gazetini, amesema dharau na kiburi ambacho mkuu huyo anakiendekeza kimesababisha hatua za kimaendeleo kushindwa kupiga hatua.

“Kama kiongozi Mkuu wa Mkoa wetu tunaomba atoke hadharani awaeleze Watanzania sababu ambazo zilisababisha ashindwe kwenda na ilikuwaje achukuwe millioni 10 alafu ashindwe kufika safari ambayo ilikuwa ya muhimu,” amesema mtoaji wa taarifa hiyo 

Hata hivyo, ziara hiyo ambayo ilifanyika Mei 26 hadi Juni 3 Mwaka huu, ambayo iliwahusisha viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza ambao walitumia kiasi cha millioni 100 kwa siku 10 walizokaa Dubai.

Katika ziara hiyo, Mulongo alipewa Sh. 10 milioni ambazo baada ya kuchukua fedha hizo inadaiwa alikwenda jijini Dar es Salaam kufanya shughuli zake binafsi na alipopigiwa simu, hakupokea wala kutoa taarifa sababu za kutokwenda safari hiyo.

Mtoaji wa taarifa hiyo baada ya kutoka katika kikao hicho, ameiambia MwanaHALISI online kuwa, licha ya kukwapua kiasi hicho cha fedha za walipa kodi ambao asilimia kubwa ni masikini, bado mpaka sasa kiongozi huyo hataki kuzungumza nao ili kueleza sababu za kushindwa kwenda safari hiyo.

error: Content is protected !!