August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DC Masale: Wavuvi wamepuuzwa

Spread the love

IMEELEZWA kuwa licha ya wavuvi wadogo kuchangia katika pato la taifa kwa kiasi kikubwa, sekta hiyo imedaiwa kupuuzwa pia kutopewa kipaumbele, anaandika Moses Mseti.

Kauli hiyo imetolewa na Moses Masale, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kwa niaba ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya kujejengea uwezo wadau kuhusu utekelezaji wa wavuvi wadogo ulio endelevu jijini Mwanza.

Mongella akizungumza katika warsha hiyo iliyoandaliwa na shirika lisilo la serikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (Emedo) amesema, sekta ya uvuvi huchangia asilimia 97 katika pato la taifa na kwamba, bado sekta hiyo imeonekana kupuuzwa hapa nchini.

“Jamii za wavuvi wadogo wameonekana kupuuzwa na kubaki nyuma bila kushirikishwa katika shughuli za maendeleo, lazima tutengeneze mazingira ya kuwaboreshea shughuli zao,” amesema Mongella.

Fatma Sobo, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi amesema, sekta ya uvuvi inachangia asilimia 2.5 ya pato la taifa na asilimia 10 ya mazao yanayouzwa nje hutokana na uvuvi.

“Sekta hii ya wavuvi wadogo ina zaidi ya wavuvi 25, 0000 lakini zaidi ya wananchi 4.5 milioni wanategemea shughuli za samaki, hivyo ni sekta muhimu kwa maendelo ya jamii na taifa kwa ujumla,” amesema Sobo.

John Makene, Mwenyekiti wa Bodi wa Emedo amesema, wavuvi wadogo hawashirikishwi katika kupanga sera zinazohusu sekta hiyo na kwamba, ni wakati mwafaka kuondoa changamoto zote zinazoikabali sekta hiyo kwa kukuza uchumi.

Mchambuzi wa Sera za Uvuvi, kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) Rome Italia, Nicole Franz amesema, Tanzania imebarikiwa kuwa na sehemu kubwa iliyozungukwa Ziwa Victoria, hivyo huwa kivutio na mfano kutoka mataifa mbalimbali kuhusu uvuvi.

Editrudith Lukanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Emedo amesema, lengo la kongamano hilo ni kuupitia mwongozo huo kuboresha uvuvi mdogo ambao unachangia kipato kwa asilimia kubwa.

“Huu ni mwongozo mpya ambao ulipitishwa mwaka 2014 Rome (Italia) kwa ushiriki wa nchi 143, lengo lake likiwa ni kutatua changamoto zinazoikabaili sekta hiyo, tunapenda wadau wakubwa kuufahamu vinginevyo hautafanikiwa,” amesema Lukanga.

error: Content is protected !!