Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa DC, madiwani Dar nusura wasichape
Habari za SiasaTangulizi

DC, madiwani Dar nusura wasichape

Spread the love

 

MADIWANI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mkoani Dar es salaam, Kisare Makore wameingia katika ‘mnyukano’ unaohatarisha maendeleo na uhai wa chama chao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mgogoro huo umefika mahala pabaya baada ya DC huyo juzi Jumatatu kunusurika kichapo kutoka kwa madiwani hao wa CCM na kusababisha kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) chama hicho wilaya ya Ubungo, kuvunjika.

Madiwani na DC hao wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu, wakimlalamikia pamoja na mambo mengine, kujenga chuki, matabaka kati yao na watendaji wa Halmashauri.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Makore alipoulizwa na alisema “waulize hao waliokuletea taarifa, mimi sijui chochote,”.

Mgogoro huo jana Jumanne, ulifika katika hatua mbaya baada ya madiwani hao kuandika barua kwa Katibu wa CCM wilaya ya Ubungo, nakala kusukumwa kwa Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Daniel Chongolo, wakimtuhumu kwa kujenga chuki na madai mengine lukuki.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika juzi Jumatatu, katika ukumbi wa Simba Oil, Kata ya Mburahati Manispaa ya Ubungo, zinaeleza madiwani wa CCM walikerwa na lugha ya dharau, kejeli na matusi kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wake, DC huyo alichukizwa namna madiwani hao walivyokuwa wakipinga taarifa yake.

Madiwani hao walihoji taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kuhusu ujenzi wa barabara zaidi ya kilometa 200 na kutaka Wakala wa barabara vijijini (Tarura), itoe maelezo pamoja na utata kuhusu umiliki wa Stendi ya Mabasi Magufuli iliyopo Mbezi Luisi.

DC Makori alionekana kukerwa na madiwani hao kiasi cha kutangaza kupambana nao hadharani, akipinga hatua yao ya kuhoji taarifa yake mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Ubungo.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na watendaji wa halmashauri akiwamo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic, wakuu wa idara pamoja na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama.

“Wakati hoja za wajumbe wa kikao hicho zikipambana moto, DC Makori kila mara alikuwa akinyanyuka kutaka kujibu alizuiliwa, lakini hata alipokuwa akijibu alikuwa na jazba sana ya mapambano na madiwani hao.” alisema mtoa taarifa wetu.

Mtoa taarifa wetu anasema kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja, alilazimika kuingilia kati kila mara lakini bado DC huyo wa wilaya alikuwa akinyang’anya kipaza sauti na kutaka kujibu kila hoja.

”Ilikuwa ni balaa katika miaka yote ambayo CCM wilaya ya Ubungo ambapo tulikuwa na madiwani lakini safari hii tumepata hasa wawakilishi sahihi ambao wakati wote wamekuwa wakisimamia misingi ya chama.

“Maana kila diwani aliyepata nafasi alihoji na kuomba ufafanuzi kwa hoja nzito na kwa mifano kutokana na taarifa iliyopo, na katika hili sisi kama wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya wilaya, hatujawahi kuona DC kama huyo ambaye anajenga matabaka kati yake na madiwani,” alisema mmoja wa madiwani hao.

”… Mchezo ulikuwa mtamu baada ya DC huyo kushindwa kujibu hoja na kuanza kuwaparamia kwa majina madiwani ambao walikuwa wanahoji sana, alinza kwa kumtaja Diwani wa Makurumla (Bakari Kimwanga), Yussuf Yenga (Mburahati), Raphael Awino (Sinza) na Eliam Manumbu (Manzese) kwamba wanafanya vikao chooni. Hapo ndipo lilipozuka balaa kumbe na yeye alikuwa amenyanyuka na Meya Jafari Nyaigesha walikwenda chooni na kupanga mikakati yao.

 

”Madiwani walikuja juu na kuhoji hatua ya mkuu wa wilaya kuwatusi na kuwadhalilisha kila mara kwenye vikao hasa vya watendaji wa halmashauri pamoja na chama na ukiangalia madiwani nao wamechoka na viongozi ambao wanastahili heshima,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao.

Wakati malumbano hayo yakiendelea, alisimama Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo, Silvester Yaredi, ambapo alitangaza kwa wajumbe kwamba amepokea barua ya malalamiko kutoka kwa madiwani dhidi ya mkuu wa wilaya.

Hata hivyo baada ya kutolewa taarifa hiyo, alisimama DC Makori na kuanza kupinga maelezo ya katibu wa chama kwamba yeye hana ugomvi na madiwani na siku moja anaweza kuondoka au kutumbuliwa au hata kupanda cheo.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumatano tarehe 19 Mei 2021

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!