Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko DC Kilosa awasimamisha kazi wenyeviti 3 wa vitongoji
Habari Mchanganyiko

DC Kilosa awasimamisha kazi wenyeviti 3 wa vitongoji

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Alahj Majid Mwanga amewasimamisha kazi wenyeviti wa vitongoji vitatu kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Mwanga amewataja wenyeviti hao waliowaondoa madarakani ni Kondo Pilipili kutoka Kitongoji cha Masugu Kati, John Kalonga – Kitongoji cha Masugu na Ally Liguta Kitongoji cha Mitalulani.

Wenyeviti hao wamesimamishwa kwa makosa ya mbalimbali ikiwemo kuuza maeneo ya hifadhi ya misitu zaidi ya hekari 70 pamoja na mashamba ya wananchi kwa wafugaji kinyume na sheria ya ardhi.

Aidha, katika hatua nyingine amemtaka mtendaji wa kijiji cha Dodoma Isanga, Andrew Kazimbaya kuripoti katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa ili akapangiwe majukumu mengine kwa kushindwa kisimamia majukumu na sheria katika kijiiji hicho.

Pia amewaagiza wataalamu wa Kata ya Magomeni wakiongozwa na Mtendaji wa kata, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mifugo na Afisa Kilimo waandae taarifa ya kina juu ya migogoro iliyosababishwa na wenyeviti na kuiwasilisha ofisi ya mkuu wa wilaya ndani ya siku saba.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ujezi wa shule ya msingi katika vitongoji hivyo kwani watoto wanatembea umbali mrefu kufuata shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!