January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DC Henjewele awatimua waandishi wa habari

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele aklihutubia wananchi wa wilaya hiyo

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele, amevituhumu vyombo vya habari vya Luninga Morogoro, akidai vikitekeleza wajibu wake, vimekuwa vikichochea, kupotosha na kukuza mgogoro wa Mauaji ya Wakulima na Wafugaji wa Vijiji Vitano vya Wilaya yake, akionya vijitazame upya. Anaandika Dany Tibason, Morogoro … (endelea).

Akijibu maswali nini hasa kinachochochea mauaji hayo, mbali ya vyombo vya habari, Henjewele ameainisha kuwa, pia wamo baadhi ya Polisi wasio Waaminifu, baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, na baadhi ya Watawala wasio waadilifu, ambao wengi wao kwa sasa wamestaafu au kufa.

Henjewele amedai, kukitokea mapigano au mauaji baada ya kulisha mazao, baadhi ya Wafugaji huvipigia vyombo hivyo vya luninga, na kueleza kuwa wanaonewa na wakulima, na kutoa taarifa hizo hewani, jambo ambalo huamsha hasira, kukuza na kuchochea mgogoro.

“Mwandishi; ninyi ndiyo tatizo, Kabla ya kutulaumu kwa kutokomesha Mgogoro wa Mauaji ya Wakulima na Wafugaji, tupongezeni kwanza kutokana na mahali tulipofika, baada ya kubaini vichocheo na Viashiria vya Mauaji hayo kwa mazungumzo.

“Mbali ya kuwahoji polepole wakulima na wafugaji mmoja mmoja, wapo Watendaji wasio waaminifu waliotajwa kuhusika na adha hiyo, ambapo wengine wamehamishwa wakati hawakutakiwa kuhama, isipokuwa kuchukuliwa hatua kali, ikiwemo kufukuzwa kazi”.amesema Henjewele.

Aidha, Henjewele amekanusha madai kuwa, aliyekuwa Diwani wa Magole, Juma Chewe (CCM), wa Kijiji cha Mbigiri, na Gervas Mtitu, wa Kijiji cha Mabwegere, hawahusiki kuchochea mgogoro huo, amedai tuhuma hizo si kweli, kwa sababu Wananchi wa Vijiji vyote vitano vinavyopakana, vinawatuhumu wafugaji kwa mgogoro na mauaji hayo.

Hata hivyo amekiri, kuna ukweli usiopingika kwamba, Kijiji cha Mabwegere kilianza kuwa na Hati za kuwa Kijiji kabla ya kuanzishwa kwa Kijiji hicho, ambapo Vyombo vya Habari, Polisi wasio Waaminifu, Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Watawala wasio na Uadilifu, ambapo wamestaafu au kufa.

Kwa Mujibu wa Barua ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu (AG) Kumbu. AGC/G.20/19/162 ya Agosti 1, 2014, Jaji Fredrick Werema, aliyomwandikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alishauri kwamba,

“Amebaini Usajili wa Kijiji kinachojiita Mabwegere chenye Usajili Na.32758 wa Desemba 8, 1989, Usajili wake una Shaka kwa sababu, kilipata hati ya kumiliki Ardhi miaka 10 kabla ya kuanzishwa, ijapo kilipata Na. MG/KJJ.552 ya Juni 16, 1999!”.ilisema sehemu ya barua ambayo Mwandishi aliiona kwa wakulima Mbigiri.

Hivi karibuni waandishi wakiwa katika ziara iliyoandaliwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu asilia (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu( Mjumita) walikuta kundi la mifugo wapata 500 wakitokea mkoa wa Iringa wakiingia wilayani humo na kukuta wamefanya uharibifu mkubwa

Lakini henjewele alipoulizwa kwa njia ya simu kulikoni mifugo hiyo kuingia wilayani humo ilhali alishapiga maarufuku alijibu kwa jeuri kuwa kwa sasa niko Dar es Salaam na hivyo waandishi hawaruhusiwi kuingia wilayani kwake bila ruhusa yake.

error: Content is protected !!