Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Dodoma ahimiza viongozi wa dini kupinga ukatili wa kijinsia
Habari Mchanganyiko

DC Dodoma ahimiza viongozi wa dini kupinga ukatili wa kijinsia

Spread the love

MKUU wa Wilaya wa Dodoma, Jabiri Shekimweli ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuhubiri upendo, amani na utulivu pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuifanya Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Ametoa ushauri huo leo tarehe 4 Desemba 2022 wakati akitoa salama katika kanisa la Karmeli Assemblies of God katika hafla fupi ya kutoa misaada mbalimbali kwa wajane, yatima na watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabiri Chande akimlisha keki mmoja wa wajane walioshiriki katika hafla ya kupatiwa huduma mbalimbali zilizotolewa na kanisa la Karmeli Assemblies of God

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo lililopo Ipagala Jijini Dodoma chini ya Askofu Mkuu Dk. Evance Chande, ameeleza kuwa sasa ukatili umeongezeka kutokana na watu kupunguza upendo na kutokuwa na hofu ya Mungu.

Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya amesema iwapo viongozi wataonesha upendo kwa jamii itasaidia kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia.

Naye Diwani wa Kata ya Ipagala, Dotto Gombo amesema kitendo kilichofanywa na kanisa kwa kuwapatia mahitaji wahitaji ni jambo ambalo linaonesha upendo wa Mungu kwa wahitaji.

“Kanisa limekuwa likifanya matukio ya kuwajali yatima, wajane na kila mwaka jambo ambalo linaonesha upendo, umoja na wale wenye uhitaji.

Naye Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk. Evance Chande amesema licha ya kuwajali watu wenye uhitaji bado kanisa linaendesha masomo ya ujasiriamali kwa lengo la kuwafanya waumini kujikwamua kiuchumi.

“Serikali haiwezi kutoa ajira kwa watu wote wanaohitimu vyuo, lakini kama vijana watafundishwa jinsi ya kujitegemea ni wazi watajikwamia kiuchumi.

“Tumeanzisha masomo hayo kwa lengo mahususi la kuhakikisha vijana pamoja na wale wenye rika mbalimbali, kuondokana na tabia ya kufikiria kupata ajira na badala yake wajiajiri wenyewe,” ameeleza Askofu Dk.Evance.

Akizungumzia suala la utoaji wa misaada kwa wenye uhitaji Askofu Dk. Chande amesema wanashirikisha uongozi wa serikali za mitaa kwa lengo la kuwapata walengwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!