Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Bukombe ataka wananchi kuchangamkia fursa hifadhi ya Taifa Kigosi
Habari Mchanganyiko

DC Bukombe ataka wananchi kuchangamkia fursa hifadhi ya Taifa Kigosi

Ofisa Uhifadhi katika hifadhi ya Taifa Kigosi, James Nahonyo akifafanua jambo wakati akizungumza na mwandishi wa habari.
Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Saidi Nkumba amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuitangaza Hifadhi ya Taifa Kigosi iliyopo wilayani humo.

Pia amewataka kutumia fursa hiyo kukuza uchumi wao kupitia hifadhi hiyo hasa ikizingatiwa lango kuu la hifadhi hiyo lipo Bukombe hivyo wasisubiri watalii kutoka mbali wakati wao pia wapo. Anaripoti Paul Kayanda, Geita… (endelea).

Nkumba amtoa wito huo juzi tarehe 14 Mei, 2022 wilayani Bukombe wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari za kata za Katente na Bulangwa kwenye bonanza lililoandaliwa mahususi kwa lengo la kuitangaza Hifadhi hiyo.

Pia limelenga kuitambulisha kwa wakazi wa Wilaya ya Bukombe na vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo ili kushirikiana katika uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

Aidha, Ofisa wa Uhifadhi wa hifadhi hiyo ya Taifa Kigosi, James Nahonyo naye ametoa wito kwa viongozi kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza hifadhi hiyo.

Amesema kuwa hifadhi hiyo ni mpya na imeanzishwa kipindi cha mwaka 2019 baada ya kupandishwa hadhi kutoka kuwa pori la akiba la Moyowos Kigosi na kuwa hifadhi ya Taifa Kigosi.

Amesema kutokana na hatua hiyo ni wazi kuwa hifadhi hiyo haifahamiki kwa watanzania walio wengi na kuna kila sababu za kuitangaza ili ifahamike.

“Wananchi wa Bukombe, wilaya na mikoa pamoja na watanzania kwa ujumla wanapewa fursa ya kuitembelea kwa gharama nafuu ya kiingilio cha Sh 4,720 kwa mtu mmoja na kwa siku moja,” amesema.

Aidha, amesema hifadhi ya Kigosi ni moja ya kivutio katika Mkoa wa Geita na wilaya ya Bukombe.

“Hivyo tuunge mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kwa kupitia hifadhi hii,”amesema.

Bonanza hilo limeshirikisha wanafunzi zaidi ya 1000 wa Kata mbili za wilaya ya Bukombe.

“Hawa ndiyo watalii wetu wazuri hapo baadaye na ni mabalozi wazuri ambao watapeleka hizi taarifa kwa wazazi na zitaenea maeneo.

“Tumeanza na hizi kata mbili lakini baadaye tutatembelea shule zote za Wilaya ya Bukombe kwakuwa asilimia kubwa hifadhi hii ipo katika wilaya ya Bukombe,” amesema.

Aidha, Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Wilaya ya Bukombe, Lutengano Mwaliba amewapongeza viongozi wa hifadhi hiyo mpya ya Kigosi kwa kukushirikisha jamii ambayo ndio wanufaika na walengwa.

Amesema zoezi hilo liwe endelevu ili kila mwananchi wa Bukombe awe na jukumu la kulinda rasrimali hiyo ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!