Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DC apiga marufuku mifugo kuingia Kilombero
Habari Mchanganyiko

DC apiga marufuku mifugo kuingia Kilombero

Spread the love

Uongozi Wilayani Kilombero mkoani Morogoro umepiga marufuku mifugo mipya kuingia wilayani humo katika jitihada za kulinda bonde la Bonde la Kilombero. Anaripoti Mwandishi wetu Morogoro…(endelea).

Marufuku hiyo imetolewa leo tarehe 13 Disemba, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hanji Godigodi wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uharibifu wa mazingira ya mto Kilombero.

Amesema baadhi ya mifugo imekuwa ikionekana karibu na kingo za mto Kilombero, wakulima wakiendesha shughuli za kilimo na wavuvi kujenga kambi zao katika bonde hilo kitendo ambacho kinaharibu mazingira ya bonde hilo muhimu kwa Taifa.

“Nimeagiza watendaji na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani hapa kusimamia wajibu wao wa kila siku wa kuwaondoa wafugaji, wakulima na wavuvi kwenye maeneo yasiyostahiki,” amesema.

Aidha, licha ya kutokuwa na idadi halisi ya mifugo iliyopo, lakini amekiri kuongezeka kwa mifugo inayoingia kinyemela wilayani humo hasa nyakati za usiku.

“Tumejipanga kwa hilo, hivi karibuni tulikamata mifugo kadhaa katika kijiji Iduhindembo ikiingia kinyemela katika wilaya yetu,” amesema mkuu huyo wa wilaya na kuongeza kuwa uamuzi juu ya mifugo iliyoko utatolewa baada ya kukamilika kwa zoezi la utumbuzi wa mifugo linaloendelea wilayani humo.

Ameongeza kuwa baadhi ya watendaji wa serikali za vijiji na kata wamekuwa wakipokea wafugaji wavamizi, ofisi yake inafuatilia suala hili.

“Ukweli ni kwamba mifugo imekuwa mingi, hii inasababisha kutokea kutoelewana baina ya wafugaji na wakulima,” amesema.

Amesema tatizo sio ofisi yake bali ni vijiji na kata ndivyo vinavyoandika barua kwake vikieleza kwamba bado wanayo maeneo kwa ajili ya wafugaji.

“Haturuhusu tu wafugaji, bali huwa tunapokea barua za muhtasari kutoka kwenye vijiji na kata zikieleza kwamba wananchi wamekubali mifugo iendelee kuingia kwenye maeneo yao,” alisema.

Hata hivyo, viongozi wa vijiji na kata waliozungumza na MwanaHalisi Online walipinga kauli hiyo wakisema kwamba wao hupokea mifugo kwa maagizo kutoka juu.

Wamesisitiza kuwa wao viongozi wa vijiji na kata hawana mamlaka ya kuruhusu au kutoruhusu mifugo, bali wenye mamlaka ni wilaya ambao ndio wanaotoa ruhusa kwa mifugo kuendelea kuingia.

Diwani wa kata ya Mofu, Greyson Mgonela amesema vijiji na kata hazina mamlaka ya kuingiza mifugo, bali wenye mamlaka ni walio juu.

Bonde la Kilombero lilitengwa kuwa Pori Tengefu kwa Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Sura ya 302 ya mwaka 1952 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 6,500.

Aidha, Serikali ilitenga bonde hilo kuwa Pori Tengefu kwa Tangazo la Serikali Namba 459 la mwaka 1997.

Serikali ilichukua hatua hiyo kutokana na umuhimu wa kimataifa na kuorodheshwa kuwa eneo la Ramsar (eneo linalopaswa kutunzwa na kulindwa tarehe 24/04/2002 na kupewa namba 1173 (W1 ItZ03).

Bonde la Pori Tengefu la Kilombero ni sehemu ya ardhioevu linalochangia asilimia 62.5 ya maji yote ya mto Rufiji hivyo kuwa chanzo muhimu cha maji kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!