Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko DC afunga viwanda vya Wachina Kibaha
Habari Mchanganyiko

DC afunga viwanda vya Wachina Kibaha

Spread the love

SERIKALI imevifunga viwanda viwili vya wachina vilivyoko Kibaha mkoa wa Pwani vinavyojihusisha na utengenezaji wa nondo na uzalishaji wa malighafi ya kutengenezea Gypsum kutokana na kukiuka sheria na taratibu juu ya usalama mahala pa kazi. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Assumpter Mshama, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amechukua uamuzi wa kuvifunga viwanda hivyo baada kubaini ukiukwaji mkubwa wa haki za wafanyakazi ikiwemo kutowapatia wafanyakazi vitendea kazi na kuwafanyisha kazi kwa muda mrefu kitendo kinachohatarisha usalama wao.

“Sisi serikali tuko pamoja na ninyi, ndio maana tumesema hebu tumeshakuwa na viwanda sasa twende tuone watu wetu wanawatumiaje, mi nilichoona leo naomba Mamlaka ya Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) we ndio una mamlaka, wameshakufa wanne, unasikia walituambia mmoja kumbe wamekufa wanne,” amesema Mshama.

Mshama ameagiza kiwanda hicho kisifanye kazi hadi pale kitakapoweka mazingira mazuri na salama kwa wafanyakazi wake.

“Na hiki kiwanda kisifanye kazi mpaka kitakapoweka mazingira mazuri ya watu ndipo kifanye kazi, kusudi la Rais John Magufuli sio viwanda tu, ni pamoja na afya za watu, tukisema tuweke viwanda ambavyo kwenu China vimekataliwa, mfano hii mashine inayotoa moto mtu anachota na mwiko kuweka mkaa wa mawe ambao nina uhakika kwenu haumtumii kweli sisi tuko nyuma kwenye teknolojia,” amesema na kuongeza.

“Lakini huwezi kutumia mtu masaa kumi na mbili akiwa kwenye moto, lakini mawe, hizo enzi za kupiga na mkono zimepitwa na wakati. Kwa hiyo hizi sehemu mbili, uko ndani hamna shida hizo sehemu mbili hazina shida osha watakuletea barua, na mimi nitafuatilia kama mmefanyia kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!