MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), imetangaa saa 12 za upungufu wa huduma ya maji kwa wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii cha Dawasa imesema, upungufu huo utatokea kwa saa 12 za leo Jumamosi tarehe 27 Machi 2021.
Sababu ya ukosefu wa majisafi ni kuruhusu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kufanya maboresho katika laini ya umeme kutoka Chalinze.
Imeyataja maeneo yatakayoathirika ni Mlandizi, Ruvu Darajani, Vikurutu, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Maili 35, Kwa Mfipa, Mwendapole, Kwa Mathias, Mkuza, Picha ya Ndege na Shirika la Elimu Kibaha.
Mengine ni, Pangani, Maili Moja, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Temboni, Kwa Msuguri, Saranga, Golani, Stop Over, Bonyokwa na Changanyikeni.
Pia, yamo maeneo ya Buguruni, Ubungo, Kisiwani, Msewe, Kilungule, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kiwalani na Pepsi mpaka Airport.
“Upatikanaji wa huduma ya maji utarejea katika hali yake ya kawaida mara tu hali ya umeme itakapotengamaa,” imeeleza Dawasa huku ikiomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Leave a comment