May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dawasa yatangaza upungufu wa maji saa 24 Dar

Bomba la maji safi

Spread the love

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (Dawasa), imetangaza upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Jumanne hadi kesho Jumatano tarehe 6 Januari 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii-Dawasa imesema, sababu inatokana na usafishaji wa machujio ya maji  hali itakayosababisha upungufu wa uzalishaji maji kwa asilimia 25 na kuathiri huduma ya maji kwa saa 24.

Dawasa imeyataja maeneo yatakayoathirika ni: Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa Ndege na Tegeta, Kunduchi na Salasala.

Maeneo mengine ni, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili na Kigamboni Navy na Ferry.

“Dawasa inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” inaeleza taarifa hiyo

error: Content is protected !!