Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dawasa: Tumuenzi Mkapa kwa Watanzania wote kupata maji
Habari Mchanganyiko

Dawasa: Tumuenzi Mkapa kwa Watanzania wote kupata maji

Spread the love

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imesema, itamuenzi Hayati Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa kwa kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mkapa, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mkapa alifariki Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshtuko wa moyo.

Mwili wake unaagwa kwa siku tatu kuanzia jana Jumapili hadi kesho Jumanne kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara kwa maziko yatakayofanyika Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Mhandisi Luhemeja akimzungumzia Mkapa amesema, yeye ndiye mwasisi wa mamlaka za maji nchini aliyehakikisha ana mtua mama ndoo kichwani.

Amesema, mwaka 1981 Serikali ya awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilianzisha Mamlaka ya Taifa ya Maji Mijini (NUWA) lengo la ilikuwa kusimamia na kutoa huduma za maji mijini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa, Jenerali Mstaafu Davis Mwamnyange akitoa heshima za mwisho

Mhandisi Luhemeja amesema, hadi mwaka 1997, NUWA ilikuwa haijafanikiwa kutoka katika mipaka ya Dar es Salaam. Hata, Dar es Salaam yenyewe yalipokuwa makao makuu ya NUWA huduma haikuwa nzuri.

Amesema, mwaka 1997, Rais mstaafu Mkapa aliivunja NUWA rasmi na kuanzishwa kwa mamlaka ya maji Dar es Salaam, Dawasa. Mkapa na Serikali aliyokuwa anaiongoza ikaanzisha mamlaka tatu za majaribio za manispaaa iwe na Mamlaka yake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa heshima za mwisho

Mhandisi Luhemeja amezitaja mamlaka hizo kuwa ni, mamlaka ya maji safi katika Manispaaa za Arusha, Tanga na Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

“Mamlaka hizi zilianza mwaka 1998. Baada ya miaka mitatu, mamlaka hizi zilifanya vizuri na mwaka 2001 ikaanzishwa sheria mpya ya maji na kila mkoa ukapewa mamlaka yake na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa mamlaka za maji nchini,” amesema Mhandisi Luhemeja.

Amesema, kwa jJji la Dar es Salaam kukatungwa sheria mpya ya maji Dar es Salaam Water supply and Sewerage Act of 2001 hapa sasa huduma ya maji ikaunganishwa na majitaka jijini.

“Hadi sasa tuna mamlaka za maji zaid ya 65 nchini,” amesema.

Bosi huyo wa Dawasa amesema, baada ya kutungwa kwa Sheria ya maji Dar es Salaam, Mzee mkapa alitafuta fedha kwa ajili ya kuboresha huduma jijini.

Amesema, mwaka 2002 Serikali ilipata mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia (WB) kiasi dola za Marekani milioni 265 na ndiyo ukaanzishwa mradi mkubwa wa Maji jijini, Dar es Salaam ‘Water Supply and Sewerage Project.’

“Hali ya huduma katika maeneo mengine bado haikuwa nzuri. Mwaka 2004 Mzee Mkapa alielekeza kiasi cha fedha Sh. 250 bilioni kwa ajili ya kutoa maji Ziwa Victoria na kupeleka maji katika mji wa Shinyanga na Kahama, miji ambayo ilikumbwa ni ukame mkubwa. Mradi huu wa Kahama Shinyanga ulitumia fedha za ndani,” amesema .

“Kwa mara ya kwanza, Serikali ilielekeza fedha nyingi kutoka katika kodi za wananchi na mapato yake ya ndani. Kwa sasa, mradi huu umepanuliwa hadi miji ya Nzega, Igunga na Tabora,” amesema.

Mhandisi Luhemeja amesema, “tunaongea sasa huduma ya maji mijini ni asilimia 84. kazi hii imefanikiwa kutokana usimamizi bora wa mamlaka za maji nchini zilizoasisiwa na Mzee Mkapa.”

“Kwa Dar es Salaam huduma inapatikana kwa asilimia 88 na Dawasa sasa inatekeleza miradi mingi kwa mapato yake ya ndani. Utamaduni wa kutumia mapato ya ndani inatokana na sera ya kujitegemea,” amesema.

Katika kusisitiza hilo, Mhandisi Luhemeja amesema, “mchango wake ni mkubwa, namna ya kumuenzi Mkapa ni kuhakikisha watu wote wanapata maji.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!