DAWA ya virusi vya corona aina ya REGEN- COV2, iliyotumika kumtibu Rais wa Marekani, Donald Trump imeidhinishwa na Mdhibiti wa Dawa Marekani kwa ajili ya watu ambao hawajawa katika hali mbaya. Inaripoti mitandao ya kimataifa.…..(endelea).
Stephen Hahn ambaye ni Kamishna wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) nchini humo, ndiye aliyethibitisha matumizi ya dawa hiyo.
Amesema, dawa hiyo ina mchanganyiko wa kingamwili mbili na kwamba, ilionesha kupunguza idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kulazwa pia kupunguza idadi ya wagonjwa wenye dalili kwenye vyumba vya dharura.

Matibabu ya kingamwili ya Regeneron ni ya pili kuhidhinishwa kwa jili ya matumizi ya dharura kutoka FDA baada ya tiba kama hiyo iliyotengenezwa na Eli Lilly kupewa idhini tarehe 9 Novemba 2020.
Leave a comment