April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dawa ya corona kutua Tanzania

Spread the love

DAWA ya ugonjwa wa corona (COVID-19), inayotengeneza nchini Madagascar, sasa itatumika nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ni kwa kuwa, Serikali ya Tanzania ina mpango wa kupeleka ndege yake nchini humo kwa ajili ya kubeba na kuleta nchini dawa hiyo, ili kutibu wananchi wake.

Rais John Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Mei 2020, wakati akimwapisha Mwigulu Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria.

Mwigulu amechukua nafasi ya Balozi Dk. Augustine Mahiga aliyefariki dunia tarehe 1 Mei 2020 mjini Dodoma. Dk. Mahiga amezikwa jana nyumbani kwao Tosamaganga, Iringa. 

Rais Magufuli amesema,  Madagascar imeiandikia barua Tanzania kuhusu  dawa hiyo, na kwamba Tanzania imeona ni muhimu kuchukua dawa hiyo na kuileta nchini kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.

“Nimewasiliana na watu wa Madagascar, kuna dawa kule ya corona wanasema wameipata, nitatuma ndege hiyo dawa ije hapa tuitumie,” amesema.

error: Content is protected !!