Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Dawa mpya za kutibu Covid-19 hizi hapa
Kimataifa

Dawa mpya za kutibu Covid-19 hizi hapa

Spread the love

 

TAASISI ya Usimamizi wa Dawa ya Ulaya – (EMA), imeidhinisha matumizi ya aina mbili za dawa za kutibu maradhi ya COVID-19, pamoja na matumizi ya dharura ya aina ya tatu ya dawa. Anaripoti Mwandishi Wetu …  (endelea).

Dawa zilizothibitishwa jana tarehe 16 Disemba, 2021 ni Sotrovimab inayozalishwa kwa pamoja na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline na Vir Biotechnology ya Marekani.

Kwa mujibu wa EMA, dawa hiyo inapunguza hatari ya wagonjwa walio na dalili hatarishi kulazwa hospitalini ama kufariki. Aina ya tatu ya dawa iliyodhinishwa kutumika kwa dharura ni Xeduvy.

EMA pia imeidhinisha matumizi ya dharura ya vidonge vya COVID-19 vya Pfizer na kusema dawa hiyo inaweza kutumika kuwatibu watu wazima walioambukizwa COVID-19 na wasiohitaji oksijeni, lakini wanaweza kupata dalili mbaya zaidi.

Kinachosubiriwa sasa ni tume ya Ulaya yenye mamlaka ya mwisho ya kuidhinisha matumizi ya dawa hizo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!