November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DART yatoa tamko kuhusu hujuma za madereva wa Udart

Mabasi yaendayo kasi

Spread the love

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema madereva wa kampuni ya mtoa huduma, (Udart) waliohusika kufanya hujuma ya kuzuia mabasi yaliyokuwa yameegeshwa katika karakana ya Jangwani, na kusababisha adha ya usafiri siku ya Jumatano ya Oktoba 10 2018, wamechukuliwa hatua. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kupitia tamko lake iliotoa leo tarehe 12 Oktoba 2018, DART imesema madereva hao wamechukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya usalama, huku ikitoa onyo kwa wafanyakazi wa mfumo wa DART watakaojihusisha na hujuma watachukuliwa hatua ikiwemo kuachishwa kazi.

“Serikali imetoa onyo kali kwa wafanyakazi katika mfumo wa DART watakaojihusisha na hujuma na kuwa hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kuachishwa kazi,” inaeleza sehemu ya tamko hilo.

Katika hatua nyingine, DART imeomba radhi watumiaji wa mabasi yanayotoa huduma katika mfumo wa DART kwa usumbufu wlaiopata, huku ikiahidi kuhakikisha kuboresha huduma zake.

error: Content is protected !!