February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DART yataja sababu za uhaba wa mabasi

Spread the love

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) imekiri uwepo wa uhaba wa mabasi katika vituo vikuu vya Kimara na Gerezani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kupitia taarifa iliyotolewa jana tarehe 26 Februari 2019 na DART inaeleza kuwa, uhaba wa mabasi katika mfumo ulianza tarehe juzi tarehe 25 Februari 2019.

Taarifa hiyo ilitaja sababu za uhaba huo, kwa kueleza kuwa unatokana na baadhi ya mabasi kufanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

“Kupungua kwa idadi ya mabasi waweza kusababisha usumbufu kwa wateja wetu. Tunaomba wateja wetu kuwa na subira wakati mabasi hayo yanafanywa matengenezo, pia tunawaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu ambao utakuwa umejitokeza,” ianeleza sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!