August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DART wafanya safari za majaribio

Spread the love

WAKALA mradi wa mabasi yaendayo haraka (Dart), leo wameanza kutoa mafunzo kwa wananchi namna ya kutumia vituo vya mabasi hayo na namna ya kulipa nauli, anaripoti Hamisi Mguta.

Ni baada ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) jana kutangaza rasmi nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi baada ya kimya cha muda mrefu.

Giliard Ngewe Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, alitangaza nauli hizo kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo – Kivukoni.

Nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

Mhandisi Mohamed Kuganda, Meneja wa Usimamizi na Uendeshaji wa Barabara Dart amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kesho katika vituo vya karibu ili kupata maelekezo jinsi ya kuanza kutumia usafiri huo.

Amesema kwa muda ambao SUMATRA walikua kimya ni kutokana na mapitio na uchunguzi wa gharama zilizowasilishwa na madereva ili kufikia gharama halisi ambazo zimeshatangazea rasmi jana.

Nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

“Ili kuingia kwenye vituo vilivyopo mwishoni ‘Terminal’ kama Kimara mwisho na vituo vilivyokua na madaraja ni lazima upande daraja hilo, lakini katika vituo vya kawaida kuna milango maalum kwa kutumia kadi maalum zitakazo uzwa na Dart kwa bei nafuu,”amesema.

Amesema kesho wananchi watatumia usafiri huo huku wakipata maelekezo na hawatatozwa chochote kwakua ni siku maalum kwa ajili ya mafunzo.

Aidha amesema kituo cha Kimara baruti ambacho kilivamiwa na basi lililokosea njia miezi michache iliyopita hakitatumika kwa kesho kutokana na matengenezo yake kutokamilika.

“Tunatumai kazi zitakapoanza rasmi kitakua tayari kimekamilika kwasababu gharama za marekebisho ni kubwa,”

“Ieleweke kwamba barabara za Mabasi ya Dart ni kwa ajili ya Mradi huo tu na hairuhusiwi chochote kupita lakini shida kubwa ni Bodaboda, Bajaji, Magari ya watumishi wa Serikali, Ambulance na Gari za jeshi, lakini natumai tutaweza kudhibiti,” amesema.

error: Content is protected !!