April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dar kupuliziwa dawa kuangamiza vimelea vya corona

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameagiza kupuliziwa dawa ya kuua vimelea vya ugonjwa wa corona (COVID-19) katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Ametoa agizo hilo alipokuwa katika Stendi ya Mabasi ya Mikoani, Ubungo leo tarehe 24 Machi 2020. Makonda amesema, ni vizuri kupulizwa dawa ikiwa ni hatia ya kukabiliana na kuenea kwa virusi hivyo.

Ameeleza kwamba, ametembeleastendi hiyo kuangalia iwapo watoa huduma wanazingatia miongozi iliyotolewa na serikali katika kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Akizungumzia msongamano katika daladala jijini Dar es Salaam, Makonda amesema ni bora kuchelewa kuliko mtu kujiingiza kwenye hatari ya kupanda daladala lililofurika na kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

error: Content is protected !!