August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Daktari ‘feki’ anaswa

Spread the love

ZACHARIA Benjamin (35), mkazi wa Morogoro amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujifanya daktari, anaandika Christina Haule.

Jeshi hilo linamshikilia Benjamin kwa tuhuma za kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kufanya kazi ya ukaguzi akiwa na mavazi ya kidaktari bila kuwa na ruhusa ya kufanya hivyo.

Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro akiwa ofisini kwake leo amesema,  mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 10 Julai  saa 11 jioni katika wodi ya wagonjwa mahututi kwenye hospitali hiyo.

Amesema, mtuhumiwa huyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa, aliingia katika hospitali hiyo na kutembelea wodi zote kuanzia wodi namna moja hadi namba 9 na baadaye kuingia wodi ya wagonjwa mahututi (Grade One).

Na kwamba, awali mtuhumiwa huyo alipofika wodi namba 7 aliamua kuingia chumba cha manesi na kuchukua koti la mganga kisha kuendelea kitembelea wodi zingine akidai kuwa, yeye ni daktari mgeni anakagua wagonjwa kama wanapata huduma ipasavyo.

Kamanda Matei amesema, daktari huyo feki alipoingia Grade One alianza kuwahoji wagonjwa hao, ndipo mgonjwa mmoja aliyekuwa na unafuu kidogo alitoa taarifa za kumshuku ‘daktari’ huyo.

Amesema, baada ya polisi kupata taarifa hiyo walipofikia na kumkamata ambapo anatarajia kufikisha mahakamani mara upelelezi utakapokalimika.

Hata hivyo,  mtuhumiwa huyo amedai kuwa, yeye alifika kwenye hospitali hiyo tarehe 10 Julai akiwa na mgonjwa wake ambaye amelazwa kwenye wodi namba 8 na kisha kuondoka kuendelea na shughuli zake.

Na kwamba, jioni ya siku hiyo alipigia simu na mgonjwa wake kuwa, hajapata huduma yoyote tangu afike hapo ndipo alipoamua kuingia hospitalini hapo kukagua hali ilivyo.

Amesisitiza kuwa, yeye ni mwanajeshi, askari wa Tanzania wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa mganga na daktari hivyo anayo ruhusa ya kuingia popote pale bila kuzuiliwa na mtu yeyote.

Hii ni mara ya pili kwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kukamata watu wanaojifanya kuwa madaktari.

 

error: Content is protected !!