May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dakika 270, Yanga bila bao

Spread the love

 

MARA baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prison, klabu ya Soka ya Yanga imetikiza dakika 27o sawa na michezo mitatu bila kupata bao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mchezo huo wa mzunguko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ulipigwa jana tarehe 9 Mei 2022, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, na kushuhudia vinara wa Ligi hiyo wakivutwa shati.

Hii inakuwa sare ya tatu mfululizo kwa Yanga kuipata yoka alipocheza dhidi ya Simba, na inakuwa pia sare yao ya sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu huu wa 2021/21, huku wakiendelea kushika rekodi ya kutopiteza mchezo wowote.

Licha ya kutopata bao kwa dakika hizo, lakini Yanga ilionekana kutengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini washambuliaji wake walikwama kuweka mpira nyavuni.

Pamoja na matokeo hayo, Yanga bado imeendelea kusalia kileleni wakiwa na alama zao 58, pointi 11 nyuma ya Simba waliokuwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 na mchezo mmoja mkononi.

Kwa sasa Yanga amebakisha michezo saba, huku kati ya hiyi minne atakuwa kwenye dimba la nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar, Coastal Union, Polisi Tanzania na Mbeya kwanza.

Michezo mitatu ya ugenini itakuwa dhidi ya Dodoma Jiji, Mbeya City pamoja na Biashara United.

error: Content is protected !!