Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dada wa Spika Ndugai afariki, azikwa
Habari za Siasa

Dada wa Spika Ndugai afariki, azikwa

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya Mary Ndugai, dada wa Spika wa Bunge, Job Ndugai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mpwapwa … (endelea).

Mary alifariki dunia Jumamosi iliyopita ya tarehe 23 Januari 2021, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Mazishi hayo ya Mary yamefanyika leo Jumatatu, 25 Januari 2021, katika makaburi ya Ving’awe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Bunge.

Akizungumza baada ibada ya kumuombea marehemu Mary iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la Mpwapwa, Waziri Mkuu, Majaliwa amewaomba wafiwa wawe na subira na utulivu katika kipindi hiki kigumu.

“Nimekuja kuungana nanyi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa Mheshimiwa Spika Job Ndugai kufuatia msiba mzito wa kuondokewa na dada yake mpendwa Mary.”

Waziri Mkuu amesema, msiba huo ni mzito na jukumu kubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema, hivyo amewaomba watoto wa marehemu, ndugu na jamaa wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai amewashukuru viongozi wa dini, Serikali na waombolezaji kwa kujitokeza na kuifariji familia kufuatia msiba huo.

Pia, amewashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa ambapo marehemu alikuwa akitibiwa.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba, Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai na baadhi ya wabunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!