February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dada wa Rais Magufuli afariki dunia

Spread the love

MONICA Joseph Magufuli, Dada wa Rais John Magufuli amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 19 Agosti, 2018 kwenye Hospitali ya Bugando iliyoko jijini Mwanza alikokuwa anafanyiwa matibabu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa za kifo hicho zimetolewa na Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kupitia ukurasa wake wa Instergram.

“Nasikitika kuwajulisha kuwa Dada wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu. Natoa pole kwa Rais Dk. John Joseph Magufuli, Familia ya Mzee Joseph Magufuli, Ndugu, Jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Raha ya milele umpe e Bwana na mwanga wa milele umuangazie, Marehemu Monica Jospeh Magufuli asterehe kwa amani, Amina,” ameandika Msigwa katika akaunti yake ya Instergram.

Kabla ya kufikwa na umauti, Monica alitembelewa na kaka yake, Rais Magufuli jana tarehe 18 Agosti, 2018.

error: Content is protected !!