Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CWT yamwomba Rais Magufuli awaache vizuri
Habari za Siasa

CWT yamwomba Rais Magufuli awaache vizuri

Deus Seif, Katibu Mkuu wa CWT
Spread the love

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimeiomba Serikali kuajiri walimu wapya, ili kuondoa changamoto ya uhaba wa walimu iliyotokana na mpango wa elimu bila malipo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, na Deus Seif, Katibu Mkuu wa CWT, wakati akieleza changamoto ya chama hicho mbele ya Rais John Magufuli, katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa CWT, jijini Dodoma.

Seif amesema, tangu Serikali kuanza kutekeleza mpango huo, mwitikio wa wananchi kupeleka watoto shule umeongezeka na kusababisha shule kuwa na uhitaji wa walimu.

“Changamoto ya pili ni ajira kwa walimu, mwitikio mkubwa wa jamii kufuatia mpango wa elimu bila malipo, umezifanya shule nyingi kuwa na utihaji wa walimu. Hivyo tunaomba hali ikiruhusu serikali iajiri walimu wapya, “ amesema Seif.

Katika hatua nyingine, Seif amesema CWT inaipongeza Serikali ya Rais Magufuli kwa kupandisha vyeo na mishahara walimu 121,534 kati ya walimu wote nchini 267,272.

“Hadi kufikia tarehe 31 Juni 2020, Serikali ilipandishia vyeo na kuwabadilishia mishahara walimu 121,534 kati ya walimu wote nchini 267,272, tunaamini kuwa kupandishwa cheo ni zaidi ya kuongeza mishahara kwa watumishi, “ amesema Seif.

Pia, Seif amesema Serikali imelipa Sh. 19.18 bilioni za malimbikizo ya madeni ya mishahara ya walimu na watumishi wnegine.

“Hadi Disemba 2019 Serikali ilipa Sh. 12.05 bilioni, aidha  tunaimani  Serikali  itaendelea kulipa kiasi kilichobaki kadri ya uhakiki utakapokamilika ili kuondoa malimbikiz ya mishahara, “ amesema Seif na kuongeza.

“Malimbikizo ya madeni ya mishahara ya Sh.19.18 bilioni walikuwa wamehakikiwa na kulipwa , tunaipongeza kwa kulipa . Ila walimu 6,000 waliokuwa wanaendelea na uhakiki wa malipo watalipwa fedha zao.”

Katibu mkuu huyo huku akishangiliwa na walimu wenzake baada ya kueleza uchaguzi mkuu ujao wana imani utakuwa wa amani, na kumwomba Rais Magufuli kuwaacha vizuri katika masilahi ya walimu nchini.

“Baada ya kusema hayo, tunakushuruku kwa kushirikiana nasi, tunakutakia majukumu mema huku tukiendela kuwakumbusha walimu kutekeleza majukumu yao, na tunaamini utatuacha vizuri, “ amesema Seif huku shangwe kutoka kwa walimu zikiibika.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE kwa habari zaidi

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!