Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko CWT Igunga: Rais Samia amerejesha ari ya walimu kufanya kazi
Habari Mchanganyiko

CWT Igunga: Rais Samia amerejesha ari ya walimu kufanya kazi

Spread the love

CHAMA cha Walimu (CWT) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, kimesema juhudi za  Rais Samia Suluhu Hassan zinatoa muelekeo chanya wa ukuaji wa sekta ya elimu nchini. Anaripoti Victor Makinda, Tabora …(endelea).

Hayo yameelezwa  jana terehe 6 Mei 2023 na Katibu wa CWT Wilayani Igunga, Sophia Maziku wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Maziku amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya elimu nchini unaleta tija na ufanisi kwenye ukuaji wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

“Kwa niaba ya walimu wilayani Igunga kwanza tunampongeza Rais  Samia kwa jinsi ambavyo Serikali yake inavyotatua changamoto za elimu kwa kujenga madarasa, nyumba za walimu sambamba na kuboresha maslahi ya walimu kote nchini.” amesema Maziku.

Amesema hatua ya Serikali kulipa malimbikizo ya madeni ya walimu, kupandisha madaraja pamoja na kuanza kurejesha utaratibu wa nyongeza ya mishahara kila mwaka, imeongeza ari ya Walimu kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

” Ahadi ya Rais Dk. Samia siku ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi, ya kwamba wafanyakazi kote nchini mambo yao yatakuwa moto kuanzia bajeti ya 2023/2024 itakayoanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu imewapa tabasamu wafanyakazi wote hususani walimu wa wilaya ya Igunga,” amesema Maziku.

Aidha, CWT wilayani Igunga imeahidi kuwa bega kwa bega na Rais Samia ambapo wamesema kuwa watamuunga mkono kwa hali na mali ili aweze kumaliza vipindi vyake viwili vya Uongozi.

“CWT Igunga tunamuhakikishia Rais Samia kuwa tupo naye bega kwa bega, tutapambana kumsaidia kwa  lolote huku tukiendelea kubaki kuwa wafuasi watiifu kwa serikali yake.” amesema Maziku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!