August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yavuka kihunzi Dimani

Kailima Ramadhan, Mkurugenza wa NEC

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimevuka kihunzi cha rufaa iliyowekwa dhidi yake na mgombea ubunge Jimbo la Dimani Zanzibar, Juma Ali Juma wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Pendo Omary.

Taarifa ya kutupwa kwa rufaa hiyo yenye kumbukumbu Na. E. A. 228/235/01/60 imetolewa na Ramadhan Kailima, Mkurugenzi wa Uchaguzi kwenda kwa mgombea wa CCM na nakala kutumwa kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la dimani na Abdulrazak Khatib Ramadhan, Mgombea wa CUF katika jimbo la dimani.

Taarifa hiyo inasomeka “Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 30/12/2016 ilipitia na kujadili rufaa yako.

Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo vilivyoambatanishwa katika rufaa yako, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekataa rufaa yako kwa sababu: “(a) Hakuna uthibitisho kuonesha fomu za uteuzi wa mgombea hazikurudishwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria. (b)

Mrufaniwa aliwasilisha barua ya utambulisho kutoka CUF yenye Kumb. Na. CUF/WMAGH/B/BS/24/16 ya tarehe 18/12/2016 kutoka kwa katibu wa wilaya ya Magharibi “B”….

“Pia fomu za uteuzi za mgombea zimegongwa muhuri na kusainiwa na Katibu wa CUF Wilaya ya Magharibi “B” – Zanzibar. Kwa sababu zilizoelezwa mrufani anaendelea kuwa mgombea,” inasomeka taarifa hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Juma alikata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Magharibi ambaye alilitupa pingamizi lake hapo awali dhidi ya Ramadhan.

Katika pingamizi hilo, mgombea wa CCM anadai kwamba mpinzani wake kutoka CUF hakupitishwa na vikao halali vya chama cha CUF hivyo hafai kushiriki katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, Fatma Gharib Haji ambaye ni msimamizi wa uchaguzi huo, amenukuliwa akisema, “mgombea wa CCM aliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF ambayo yalitupwa, baada ya kuonekana hayakuwa na mashiko. Hatimaye wagombea wote wakapewa fomu za kuwapitisha.”

error: Content is protected !!