October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yasaka watia nia ya urais

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Spread the love

MWISHO wa kuchukua fomu kwa ajili ya watia nia ya urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), sasa ni tarehe 30 Juni 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Awali chama hicho kilieleza, kuwa mwisho wa kuchukua fomu kwa watia nia ya kugombea kuteuliwa kugombea nafasi hiyo (urais) ingekuwa tarehe 16 Juni 2020, lakini mpaka juzi ni makada wawili tu waliojitokeza.

Juma Kilaghai, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho Taifa amesema, uamuzi wa CUF kusogeza mbele muda wa kuchukua fomu, ni kutoa fursa zaidi kwa walio na nia ya kujitokeza.

“Tumeona hakuna sababu za msingi za kutusukuma kufunga zoezi hili haraka, lakini hapa kati kulikuwa na mambo mengi na watu walikuwa na shughuli nyingi,” amesema Kilaghili.

Ofisa huyo wa CUF amesema, mpaka kufika tarehe hiyo, waliokuwa na dhamira ya kujitokeza watakuwa wamepata muda wa kutosha kujitafakari na kufanya uamuzi sahihi.

Kilaghai amesema, tayari watia nia wawili wamejitokeza kuchukua fomu, mmoja akitoka Tanzania Bara na mwingine visiwani Zanzibar.

error: Content is protected !!