December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yapata katibu mkuu mpya

Spread the love

BARAZA Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) limempitisha Haroub Shamis kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Shamis anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Khalifa Suleyman Khalifa aliyefariki dunia tarehe 30 Machi 2020 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 na naMohamed Ngulangwa,Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kupitia taarifa yake kwa umma.

Amesema, awali, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipendekeza majina ya wajumbe wawili wa Baraza Kuu kwenye kikao cha baraza hilo ili wapigiwe kura kama inavyoelekezwa na Katiba ya CUF Ibara ya 96(1).

Marehemu Khalifa Suleyman Khalifa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF

Ngulangwa amesema, wajumbe waliopendekezwa ni Hamida Abdallah Khuweshil na Haroub Mohamed Shamis na walipopigiwa kura na Baraza Kuu.

Amesema, Hamida alipata kura 27 na Haroub alipata kura 33 na kura 2 ziliharibika.

Haroub aliyezaliwa tarehe 5 Machi 1962, alikuwa Mbunge wa Choga kati ya mwaka 2010-2015 kupitia chama hicho.

Ngulangwa amesema, Baraza Kuu limemaliza vyake na Maazimio ya Baraza Kuu yatawekwa hadharani kupitia mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika muda utakaobainishwa baadae.

error: Content is protected !!