January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yamtega Rais Samia kuhusu Mbowe, yaanza mikakati uchaguzi 2025

Spread the love
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ifute kesi zinazowakabili wanasiasa, ikiwemo ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumi Uchumi, Dar es Salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 4 Desemba 2021 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Mhandisi Mohammed Ngulangwa.
“Mwaka huu tumeshuhudia viongozi wa vyama vikuu vya upinzani wakisota gerezani kwa kesi nzito yenye kugubikwa na utata mzito, ikiwa  pamoja na kesi ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Sasa ni wakati muafaka wa kufuta kesi za kubambikiza za viongozi wa kisiasa na kufanya mamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa,” amesema Mhandisi Ngulangwa.
Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 Desemba 2021, Mhandisi Ngulangwa ameiomba Serikali ya Rais Samia, iimarishe maridhiani ya kitaifa, pamoja na kuunda tume huru ya uchaguzi.
“Tunatoa wito kwa Rais Samia kutumia maadhimisho ya miaka 60 uhuru wa Tanzania Bara kuwarudishia Watanzania uhuru na furaha ya kweli, ni muda muafaka wakurudisha demokrasia na kuimarisha kuanzia muafaka wa maridhiano na katiba nchini. Muda mufaka kufanya mchakato wa kupata tume huru ni kuwafanya Watanzania  kuchagua viongozi wanaotaka,” amesema Mhandisi Ngulangwa.
Wakati huo huo, Mhandisi Ngulangwa amewataka viongozi na wanachama wa CUF, kujiandaa na chaguzi za ndani za chama hicho, ili kujipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
“Napenda kuwakumbusha viongozi kuzingatia kalenda ya uchaguzi ndani ya chama unaostahili kuanza mapena iwezekanavyo kwenye matawi yetu ya chama nchi nzima, ni muda muafaka kuimarisha na kuanzisha matawi mapya kwa kuzingatia katiba ya chama. Ikumbukwe kwamba, matawi imara yatatusaidia kupata mtandao imara wa chama kuekeka uchaguzi wa  Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024, hatimaye Uchaguzi  Mkuu wa 2025,” amesema Mhandisi Ngulangwa.
error: Content is protected !!