Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF yamtaka Rais Samia “atembee kwenye maneno yake kwa vitendo”
Habari za Siasa

CUF yamtaka Rais Samia “atembee kwenye maneno yake kwa vitendo”

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, atimize ahadi yake ya kujenga maridhiano na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi, kwa kuhakikisha tume huru ya uchaguzi inapatikana kabla ya chaguzi zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, tarehe 28 Novemba 2022, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema upatikanaji wa tume hiyo ni muhimu katika kufikia lengo la kuwa na siasa za kistaarabu pamoja na maamuzi ya wananchi kuheshimiwa.

“Nilikuwa navutiwa na kauli ya Rais Samia pamoja na sera yake ya maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na ujenzi mpya wa taifa. Ni muhimu atembee kwenye maneno yake kivitendo, tuelezwe mpango kazi wa kupata tume huru ya uchaguzi,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amesema anatiwa shaka na hatua ya Serikali kutoweka mpango mkakati wa kupatikana kwa tume hiyo, licha ya Kikosi Kazi Cha Rais Samia kuwasilisha ripoti yake iliyobeba maoni ya wadau kuhusu maboresho ya demokrasia ya vyama vingi.

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

“Mchakato wa katiba mpya ni muhimu lakini uchagu,I hauwezi kuahirishwa lazima tupate tume huru ya uchaguzi ambayo itaweza simamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Napata wasiwasu mpaka Sasa hivi sijasikia kama Baraza la mawaziri limekutana kujadili mpango kazi wa kutekeleza haha mambo muhimu ya kupata Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,” amesema Prof. Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa CUF amesema “muda unakwenda maamuzi yasipofanyika tunaweza tukajikuta tunaingia 2024 kwenye uchaguzi yanarejea yaliyotokea 2019 wagombea wengi walienguliwa hawakupata fursa ya kuweza kushiriki uchaguzi mkuu.”

Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba ameiomba Serikali ya Rais Samia iweke wazi mpango kazi wa kutekeleza mapendekezo ya wadau yaliyokusanywa na kikosi kazi, ikiwemo ya ukamilishaji mchakato wa kupata katiba mpya, kufunguliwa mikutano ya hadhara, ushiriki wa wanawake katika siasa, maboresho dhidi ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria za uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba amewataka wananchi kudai haki ya kufanya siasa na demokrasia ya kweli Kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!