Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF yampuuza Prof. Lipumba
Habari za SiasaTangulizi

CUF yampuuza Prof. Lipumba

Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar. Picha ndogo, Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

NASSOR Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar amesema Katiba ya chama hicho haimpi mamlaka yoyote Profesa Ibrahim Lipumba kutengua uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wakurugenzi kama alivyotangaza, anaandika Pendo Omary.

Prof. Lipumba amabaye anajiita mwenyekiti wa CUF huku akiungwa mkono na Msajili wa Vyama Vya Siasa juzi alitangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wote kwa upande wa Zanzibar.

Lipumba pia alitangaza kumsimamisha Maalim Seif Hamad Sharif, Katibu Mkuu wa CUF kwa  kile alichokiita kutofika ofisi kuu za chama hicho Buguruni, jijini Dar es Salaam ili apewe maelekezo na mipango ya ya ujenzi na uimarishaji wa chama.

Akizungumza leo asubuhi na waandishi habari mjini Unguja, Zanzibar Mazrui amesema, “hakuna Ibara yeyote ya Katiba ya CUF inayompa mamlaka ya kuwatengua wakurugenzi na manaibu wakurugenzi au viongozi wengine wa chama.”

“Ibara ya 85 (11) – kuhusu Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa, inasema kuwa mwenyekiti anaweza kumsimamisha kazi Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi kwa utovu wa nidhamu au kushindwa kazi na kulitaarifu Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa uamuzi wa mwisho.”

Amesema kipindi cha uongozi wa chama kwa viongozi waliochaguliwa kitakuwa miaka mitano (5) kwa ngazi zote isipokuwa kama kiongozi huyo ameshindwa kazi aliyopewa.

“Lipumba amekurupuka. CUF ni taasisi imara, si kikundi cha wahuni kama yeye na genge lake wanavyojidhihirisha. Lazima utaratibu wa kikatiba uzingatiwe,” amesema na kuongeza;

“Tulipokea ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu zetu kutoka kwa Magdalena Sakaya tarehe 4/3/2017 majira ya saa 6 za usiku na tumemjibu kwa barua yenye maelezo yanayojitosheleza kwamba; “Hatukuona uhalali wa kikao hicho ulichotutaka tuhudhurie,” amesema Mazrui.

Amefafanua kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya CUF Ibara ya 84 (1) ikisomwa pamoja na Ibara ya 93 (1)(d) mwenye mamlaka ya kuitishwa kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Katibu Mkuu ambaye yupo Ofisini Makao makuu Mtendeni, Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!