November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yampigia goti Rais Magufuli 

Spread the love

CHAMA Cha Wananchi (CUF), kinaugulia maumivi ya kutofanya mikutano ya kisiasa hasa muda huu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Maumivu hayo yameelezwa na Salvatory Magafu, Naibu Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho wakati akizunguza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Magafu ameeleza kwamba katazo la mikutano ya hadhara lililotolewa na Rais John Magufuli, limeathiri shughuli za mikutano na kumwomba rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu asitishe katazo hilo.

“Huu ni muda muafaka wa kuruhusu mikutano,” amesema Magafu na kuongeza “uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu.”

Ofisa huyo wa CUF ameeleza kuwa, katazo hilo linakwenda kinyume na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 na kinyume na matamko ya Umoja wa Afrika katika kutetea uhuru wa kueleza.

“… ni kinyume cha sheria nyingine za nchi hii na matamko ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ambayo sisi kama nchi, wanachama tumesaini na kuridhia, tunamsihi Rais Magufuli kuruhusu wakati huu tuanze kufanya mikutano ya kisiasa,” amesema Magafu.

Hata hivyo, Magafu amesema Jaji Francis Mutungi ambaye ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ameeleza kutokuwa na barua ya chama chochote cha siasa kulalamikia kutofanya mikutano.

error: Content is protected !!