Saturday , 20 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

CUF yamjibu Mtatiro

Spread the love

TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa 24/October/2018

Kuhusu ufafanuzi wa Mtatiro kufuatia Mazungumzo yake na Wanahabari yaliofanyika Kisiwa cha Unguja .

CUF-Chama cha Wananchi kinayachukulia Mazungumzo yale pamoja na ufafanuzi wake unaotapakaa kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii kama ni sehemu ya Mbio za kutaka nafasi ya Ajira kupitia Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Ndugu Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mtakumbuka kua Mtatiro alipohama kutoka Cuf na kujiunga na CCM moja ya sababu alizotoa ni pamoja na kutafuta Jukwaa sahihi la kufanyia sasa ili aweze kufikia Mustakbali mwema wa Kisiasa kama ambavyo wamefikia Wanasiasa wadogo ambao wamepitia kwenye Jukwaa sahihi la Kisiasa.

Kama hilo ndio lengo la kujiunga kwake na CCM bila shaka yote anayofanya hivi sasa yatabaki na lengo lile lile la kutafuta mustakbali wake mwema Kisiasa..

Kuhusu ufafanuzi wa hoja zake.

1 Kuhusu yeye kuitwa Kafiri kipindi yupo Cuf ni hoja dhaifu kwakua alipaswa kulieleza hilo kipindi kile kile alipokua Cuf ili hoja yake iwe na mashiko . Vikao vya Chama ndivyo venye uwezo wa kushughulikia masuala ya Nidhamu ya Wanachama na si vinginevyo na kwa bahati nzuri kipindi hicho anachokisema, yeye Mtatiro alikua ndie Naibu Katibu Mkuu Bara kwa hivyo hakua na tatizo la kuandaa na kuitisha Kikao kwa mujibu wa Katiba ya Chama ili kushughulikia tatizo tajwa kwenye ufafanuzi wa hoja zake.

2. Lipumba kuivuruga Cuf, hata hili nalo ni tatizo ambalo yeye Mtatiro ndie alieanzisha tatizo hili kwa kutoheshimu Katiba ya Cuf.

Mtakumbuka kua Mtatiro ndie aliekua Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu Maalum uliojadili pamoja na mambo mengine lakini pia ulijadili BARUA YA KUJIUZULU KWA PROFESA LIPUMBA NAFASI YA MWENYEKITI TAIFA.

Mtatiro kwa kutii maelekezo ya Maalim Seif alikiuka Katiba ya Cuf katika kuendesha Mkutano ule na kupelekea kuvunjika. Mtatiro ndie aliekua anamshauri vibaya Katibu Mkuu na ndie aliechangia kutufikisha hapa tulipofika.

Kwenye Mgogoro wa Cuf Prof Lipumba hoja zake zipo wazi katika Chama. Prof alihitaji Chama kiongozwe kwa mujibu wa makubaliano ya Vikao na sio utashi wa mtu Mmoja jambo ambalo yeye Mtatiro alimpinga Lipumba kwakutegemea kua atapoondoka Lipumba yeye ndie ataepewa nafasi hiyo.

Watanzania na Wanahabari mnalijua vyema sakata la hili na hapa lilipofikia.

2015 Mwezi August Profesa aliandika barua ya kujiuzulu kama ishara ya kupinga Maamuzi ya mtu mmoja ndani ya Chama baadhi yetu pamoja na kushauri hatua za kuchukua ili kukinusuru Chama kwenye mgogoro mzito ambao ungeweza kutokea lakini sie tukaonekana wasaliti.

Leo Mtatiro anakuja na hoja ya kua eti Lipumba ameivuruga Cuf,Mara Maalim Seif ni zaidi ya Cuf kwenye Cuf, hivi haya anayajua baada ya kuukosa Uenyekiti wa Cuf ?

Kifupi hoja zote hizi zinazo husu Lipumba na Maalim ni katika Mwendokasi wa kutafuta ajira na si vinginevyo .

3. Kuhusu Cuf kua sio Taasisi imara, hii nayo ni hoja dhaifu sana. Cuf ni Taasisi imara inayoendeshwa kwa mujibu wa Katiba na ndio maana hata pale Mtatiro na Maswahiba zake wanapojaribu kuturejesha nyuma kwa kufanya mambo kinyume na Katiba ya Chama.

Wanachama wamekua imara kupinga ukiukwaji wa Katiba ya Chama na hatimae kina Mtatiro kujikuta wamekimbilia Mahakamani kufungua Kesi mbalimbali za kikatiba. Mfano, Mtatiro mwenyewe kujiita kua Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi cheo ambacho hakipo kwenye Katiba ya Cuf huku wapambe wake pamoja na Maalim Seif wakibariki ukiukwaji huo wa Katiba ya Cuf .

Kama Cuf isingekua Taasisi na isingekua imara basi ukiukwaji huo ungekubaliwa kama ambavyo yeye Mtatiro anaukubali mpaka leo. Mtatiro wakati anajiunga na CCM alisema kua anatoka Cuf akiwa na Cheo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi cheo ambacho hakipo kwenye Katiba na Mtatiro anafahamu kua kwa mujibu wa Katiba ya Cuf hakuna Cheo hicho.

Mwisho Watanzania na Wanahabari mnakumbuka kua kwenye suala la UKAWA Prof Lipumba na Dr Slaa walipinga kuwafanya wale waliotupima kwenye Bunge la Katiba kua ndio Wagombea kwenye UKAWA na hasa kwenye nafasi ya Mgombea wa Urais. Hii ndio hoja ya Profesa ambayo Mtatiro na wenzake waliipinga sana. Mtatiro alipata kusema kwamba yeye kwa upande wa Cuf ndie aliekua anaiwakilisha Cuf kwenye Think Tank ya UKAWA.

Leo Mtatiro anasahau na kuanza kuuponda UKAWA ambao yeye ndie miongoni mwa Think Tank ya UKAWA? Kisha mtu huyu anajilinganisha na Prof Lipumba kwa uwezo wa kufikiri na kuona mbali katika matukio ya Kisiasa?

Prof ameona tatizo la UKAWA tangu Mwaka 2015, Mtatiro anaona tatizo la UKAWA 2018 yani kilichoonwa na Prof Lipumba 2015 Mtatiro anakiona Miaka mitatu baadae?

Kwa tofauti hii ya maono Mtatiro hawezi kulingana na Prof Lipumba kwa namna yoyote ile.

Suala la Seif kua ni zaidi ya Cuf ndani ya Cuf ni hoja ambayo Mtatiro aliipinga tangu awali wakati mgogoro huu unaanza.

Kuhusu Maalim Seif kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wale aliowaita wafuasi wa Lipumba ni kinyume cha Katiba ndio maana pengine Maalim alishindwa kufanya hivyo kwakua Mtatiro hakua na hoja za msingi dhidi ya wale aliowaita wafuasi wa Lipumba. Hivi unamshauri Maalim Seif awafukuze watu kwakua tu wanaunga Mkono hoja za Lipumba kuhusu UKAWA ?

Mtatiro anaendeshwa zaidi na utashi wa kupata ajira Serikalini lakini katika kufikia lengo hilo anakosa busara na Hekima. Mie namfananisha na mtu asie tafakari kabla ya kuandika au kuongea kitu.

Busara ni kufahamu kitu cha kuandika au kuongea lakini hekima ni kufahamu wakati wa kuandika au kuongea. Ni Mtatiro huyu huyu alikosoa Bajeti ya 2018/2019 kwa nguvu kubwa zilizojaa mbwembwe za kila aina mpaka kusema maneno yaso hata nidhamu kwa rais wa Nchi lakini mwezi mmoja na nusu akasahau yote na akaamua kuunga Mkono jitihada za Rais katika kusimamia Maendeleo ya Nchi yetu. Hapa utagundua kwamba kikichopo ndani ya nafsi yake ni mbio za kutafuta Ajira na si kuunga Mkono jitihada za Rais. Ni kweli Wapinzani moja ya wajibu wetu ni kukosoa, lakini ukosoaji wetu unajenga umoja? Una heshima na utu wa mtu? Au unalenga kutafuta umaarufu na kujipandisha thamani ili wanunuzi wafike Bei ?

Kwa hakika hapana hoja kwenye ufafanuzi wa Mtatiro bali pana Viroja. Maalim Seif anavuna alichokipandakwa Mtatiro.

Abdul Kambaya
Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma CUF

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!