July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CUF yakwama tena kortini

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesikiliza hoja za kupinga kiapo cha ushahidi kilichotolewa na Muhidin Thabit, shahidi wa Kondo Bungo katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge kwenye Jimbo la Mbagala, anaandika Faki Sosi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Bungo, aliyekuwa Mgombea Ubunge kwenye jimbo hili kupitia Chama cha Wananchi (CUF) dhidi ya Issa Mangungu, mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bungo amewasilisha mashahidi mahakamani hapo ambapo kiapo cha Thabit (shahidi wa Bungo) kimepingwa na upande wa walalamikiwa kwa madai kuwa, ndani ya kiapo hicho kuna ushahidi wa uongo.

Mbele ya Richard Kidela, Jaji wa Mahakama Kuu anayesikiliza kesi hiyo Kisutu, Samson Mbamba, wakili wa upande wa mlalamikiwa (Mangungu) amesema kuwa, aya ya tano ya kiapo hicho shahidi ametaja kuwepo kata nane wakati kwenye orodha ameandika kata tisa.

Mbamba amesema kuwa, ushahidi huo ni wa oungo ambapo ameiomba mahakama isiupokee ushahidi huo.

Nassor Juma, wakili wa mlalamikaji amesema kuwa, shahidi huyo ametoa ushahidi wa kile anachokijua kuhusu ushahidi wake na kuwa yale aliyoyaacha ni kwamba hayajui.

Jaji Kidela ameahirisha kesi hiyo na kwamba uamuzi wa kiapo cha shahidi huyo utatolewa kesho.

error: Content is protected !!