July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF yaipopoa serikali

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Amina Amour (CUF) amesema, serikali haina nia ya dhati ya kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Amina amesema serikali imekuwa ikitenga fedha katika bajeti yake kwa ajili ya mfuko huo lakini haizipeleki katika halmshauri.

“Serikali haioni kwamba hii ni kama vile kuwadanganya wanawake kwa kuwa, haina nia ya dhati ya kuwasaidia wanawake na kuwaacha wateseke,”? Amehoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu amesema, serikali inayo dhamira ya dhati ndio maana mwaka 1998 iliufufua mfuko huo wa wanawake.

‘Kuanzia mwaka huu tumeanza kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa wanawake, lakini pia halmashauri zinatakiwa kutenge asilimia tano katika bajeti yake kwa ajili ya  mfuko huo badala ya kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu,” amesema.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Omar Juma, Mwalimu amesema mwaka 2013/14 serikali ilitenga Sh. Bil 2 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake lakini fedha zilizotolewa ni Sh. Mil 515.6.

Amesema, mkakati wa serikali ni kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko huo ambapo kwa mwaka ujao wa fedha 2015/16 Sh. Bil 1.5 zimetengwa na mikoa yote 25 ya Tanzania Bara imenufaika na fedha za mfuko huu.

Mwalimu amesema kuwa, halmashauri katika mikoa ilipatiwa fedha na wizara kwa viwango tofauti kwa kuzingatia maombi kutoka halmashauri husika na urejeshaji wa fedha hizo kabla ya kupatiwa nyingine.

Katika swali lake Juma alitaka kujua mikoa iliyofaidika na mfuko huo na mikakati ya kuhakiksha fedha zinazotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake zinatolewa zote.

error: Content is protected !!