July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF wazidi kuikomalia ZEC kuhusu uchaguzi

Spread the love

WAJUMBE wa Baraza la wawakilishi wa Zanziba kupitia Chama cha Wananchi (CUF), wameitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kutengua tamko la mwenyekiti wa tume hiyo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mwakilishi mteule wa Jimbo wa Mgogoni Abubakar kwa niaba ya wawikilishi hao 26  

Amesema kuwa mwenyekiti huyo amekwenda kinyume na katiba na sheria ya nchi hiyo kwa kufutamatokeo hayo.

Khamis amesema kuwa uchaguzi ulifanyika vizuri na kuwapa nafasi wananchi wa Zanzibar waliojiandikisha katika daftari la kudumu kuchagua kiongozi wanayemtaka na baadaye upigaji kura ulipomalizika kazi ya kuhesabu ilikwenda vizuri matokeao yalitangazwa kwa kila jimbo pia hakukuwa na malalamiko ya chama chochote cha kisiasa kilichoshiriki kwenye uchaguzi huo.

Aidha aliongeza kuwa kuwasheria ya Uchaguzi Zanzibar namba 11 ya mwaka 1984 imetoa uwezo na mamlaka ya kusimamia na kuendesha uchaguzi wawakilishi na masheha(Madiwani)kwa msimamizi wa jimbo .

“Hakuna sehemu yoyote katika katiba ya Zanzibar ya 1984 inayotoa mamlaka kwa mwenyekiti tume ya uchaguzi au msimamizi wa uchaguzi kufuta matokeo halali ya uchaguzi” amesema Abubakar Khamis Bakari.

Amesema kuwa imewashangaza sana kuona uchaguzi huo umeenda sambamba na ule wa wabunge wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania na kutumia daftari moja la kujiandiandikishia wapikura ikiwa uchaguzi mmoja unadosari mwengine hauna dosari inaitashaka.

Wawakilishi walioandamana naye ni pamoja na wa majimbo ya Mto Pepo, Malindi, Chukwani, Mgogoni, Ole, Kijini, Wingwi, ChakeChake, Micheweni, Gando, Chambani, Mtambile, Tumbe, Mwembe Kwelekwe, Mpendae, Wete, Chonga, Kiwani Ziwani, Kojani, Bumbwini, Mkoani, Wawi, Mtambwe, Nungwi na Konde.

error: Content is protected !!