July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF wapigania ushindi wa Chadema

Spread the love

MGOMBEA udiwani Kata ya Makurumla, Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CUF, Omary Thabit amesema mwaka huu wananchi wa jimbo hilo wanabahati kubwa kupata wagombea mashuhuri akiwemo mgombea Ubunge wa Chadema, Saed Kubenea kwa kuwa ni mtu aliyeanza harakati za kufuatilia maslahi ya wananchi kwa muda mrefu. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na mwanaHALISI Online Thabit amesema mgombea huyo alianza kuonyesha hisia za ukombozi akiwa kama mwandishi mahiri wa habari za uchunguzi kabla ya kugombea ubunge katika jimbo hilo hivyo ataliwakilisha vizuri jimbo lake pindi wananchi watakapompa ridhaa ya kuwa Mbunge.

Thabit anagombea Udiwani katika kata hiyo akiwa na wapinzani sita, anaamini kama Kubenea aliweza kupigania maslahi ya taifa kwa kutumia kalamu yake akiwa kama mwandishi mwanaharakati, hivyo ataweza pia kulitumikia Jimbo lake kwa kutumia mdomo wake wa kusemea matatizo wananchi wake na kufichua maovu Serikalini.

Katika kata hiyo Thabit anayefahamika kwa jina lingine la ‘Kijiko’ anapinzana na Wagombea hao sita akiwemo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Hassan, Silvester Ruben kutoka ACT-Wazalendo, Khadija Jabir wa Chama Umoja na Maendeleo (CHAUMA), Issa Omary wa Tanzania Labour Party (TLP), Salima Khalfan, (JAHAZI ASILIIA) pamoja Neema Kasim wa UMD.

Thabit namzungumzia Mgombea Rajabu Hassan kama mgombea aliyepata uongozi mara kadhaa kwa njia ya rushwa ambaye ameongoza kwa miaka 15 bila ya kuleta maendeleo yeyote katika kata hiyo hasa katika suala la Maji ambalo alishawahi kulisema katika mikutano yake kuwa hakuna diwani yeyote atakayeweza kuleta maji katika kata hiyo kwa kuwa suala la maji ni sugu.

Suala la kutatua tatizo la maji katika kata hiyo ni kipaumbele cha tatu kwenye orodha ya viapaumbele vya vya Thabit ambapo amesema licha ya mgombea udiwani wa CCM kusema kuwa tatizo hilo ni sugu, atahakikisha anarudisha miundombinu ya maji palipo na miundombinu chakavu na kuchimba visima.

“Kwa kushirikiana na wadau na wafanyabiashara mbalimbali nitaanzisha visima vitatu vya kisasa vyenye kina cha kawaida ambavyo vitaweza kuhudumia watu zaidi ya elfu tano kwa kila kimoja ili wakazi wangu wenye jumla ya takriban 200,000 waweze kunufaika na huduma hii” anasema Thabit.

Anasema kwa kumtumia fulsa ya Mbunge wake Saed Kubenea kufikisha kero mbalimbali bungeni atahakikisha anaweka miundombinu ya barabara katika mitaa sita ya kata na kukuza elimu kwa kuondoa michango isiyokuwa ya lazima katika shule tatu za msingi za Mianzini, Dokta Omary na Karume.

Kata hiyo ina shule moja ya Sekondari ya Makurumla ambayo Thabit anasema ni shule ambayo inamatatizo mengi ambayo anatarajia kuyatatua akipewa ridhaa ya kuwa diwani akiongozana na mbunge wake kubenea.

“Saed Kubenea anagombea Ubunge, atakuwa lulu ya Taifa zima na sio jimbo la Ubungo tu kwakua anauwezo wa kujenga hoja na kutetea wananchi wake.” Anaseema na kuongeza

“ni mtu jasiri mwenye uwezo wa kujenga hoja na kikubwa ni kwamba nitasikitika sana wananchi wa Jimbo la Ubungo wakikosea kuchagua watakua ni miongoni mwa watakaopata Dhambi kwa mungu”anasema Thabit.

error: Content is protected !!