July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF wainanga CCM Kondoa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliye pia Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya

Spread the love

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliye pia Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya, amesema kuwa umasikini uliokithiri kwa Watanzania unatokana na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Sakaya ametoa kauli hiyo jana, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi mjini Kondoa, Dodoma, akiambatana na viongozi wa kitaifa kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura.

Amesema serikali haina nia njema ya kuwaandisha wananchi katika daftari hilo. Kwamba, kuna mipango ambayo inafanywa na wanachama wa CCM kwa lengo la kutaka kununua vitambulisho vyao ili wasiweze kupiga kura wakati ukifika.

Naye mbunge wa Viti Maalum, Moza Said, amesema licha ya Kondoa kuwa mji wa kihistoria na wilaya kuwa na umri wa miaka 89, lakini wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba mkubwa wa maji.

Amesema Kondoa imekuwa ni wilaya ambayo iko nyuma kimaendeleo sambaba na kuwa ya mwisho kielimu kutokana na utawala mbovu wa CCM ambao unalenga kuwadidimiza wananchi ili wasiweze kutambua ukweli.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Taifa, Abdul Kambaya, amesema kuwa anasikitishwa na mipango ya serikali ya kutaka kuwagombanisha Watanzania masikini huku vigogo wakiendelea kuponda raha.

“Serikali imeratibu mpango wa kuligombanisha Jeshi la Polisi na wananchi bila wao kutambua kuwa hao ni masikini wenzanzao. Ndugu zangu, nataka niwambie kwa sasa wananchi wamekuwa na chuki na jeshi la polisi kutokana kuwapiga wakitekeleza amri za wakubwa wao,”amedai Kambaya.

error: Content is protected !!