July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF: Serikali inaandaa vurugu

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Abdual Kambaya (wa pili kulia)

Spread the love

SERIKALI imedaiwa kuandaa vurugu wakati wa kupiga kura za maoni na uchaguzi mkuu mwaka huu. Anaandika Pendo Omary …. (endelea).

Kauli hiyo imetolewa  leo jiji Dar es Salaam na Adual Kambaya- Naibu  Mkurugenzi wa habari wa uenezi wa Chama cha Wanananchi (CUF) katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Kambaya amesema “CUF inajua kutakuwa na vurugu zilizoandaliwa na serikali yenyewe”.

“Hivi juzi akiwa kwenye Chuo cha Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, alimuomba Rais Jakaya Kikwete aongeze fedha kwani kuna vifaa vipya wameviagiza na wanahitaji kuvifanyia mazoezi. Bila shaka ni silaha kwa ajili ya uchaguzi na kura ya maoni,” amesema Kambaya.

Ameongeza kuwa Rais Kikwete alilitaka Jeshi la Polisi likae mguu sawa kuelekea kura ya maoni.

“CUF tunamwambia Kikwete kwamba huu sio muda wa vitisho bali anapaswa kuangalia hali halisi na kufanya maamuzi sahihi na kuwa mkweli kwamba BVR haiwezekani kuwahi tarehe ya kura ya maoni,” ameongeza Kambaya.

Mbali na Rais Kikwete kuhadharishwa pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa itamke kushidwa na kutokuwepo uwezekano wa kura ya maoni ili kuepusha taifa kuingia gharama za kutumia fedha nyingi kuandaa kura hiyo.

Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uandikishaji nchi nzima utaanza siku sita kuanzia leo na kusisitiza kuwa kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa itafanyika 30 Aprili mwaka huu.

Utafiti uliofanywa na CUF unaonesha, BVR moja inaandikisha chini ya watu 60 kwa siku. Lengo la NEC ni kuandikisha wapiga kura 80 mpaka 100 kwa siku.

“Kitendo cha serikali kuazima BVR nchini Nigeria na Kenya inaonesha wazi kwamba, kwanza haikuwa imejiandaa kabisa kwa hili zoezi.  Zimebaki siku 34 kura ipigwe na BVR 7750 hazijanunuliwa,” ameongeza Kambaya.

error: Content is protected !!