Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CUF Lipumba; Tumeathirika
Habari za Siasa

CUF Lipumba; Tumeathirika

Spread the love

UAMUZI wa kufutwa kwa Bodi ya Chama cha Wananchi (CUF) uliotolewa jana tarehe 18 Februari 2019 na Jaji Benhajj Masoud kutaathiri shughuli za chama hicho. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Akizungumza na mtandao huu Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya CUF Kambi ya Prof. Ibrahim Lipumba amesema, miongoni mwa athari zake kutofanya kikamilifu shugguli za chama kwa kukosa ruzuku.

Kambaya ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kufuta wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya CUF iliyoteuliwa na Prof. Lipumba ambayo imeelezwa, ilikiuka Katiba ya chama hicho.

Uamuzi huo ulitolewa kufuatia Ally Saleh, Mbunge wa Malindi na mfuasi wa Kambi ya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho kufungua kesi namba 13 ya mwaka 2017 kupinga bodi iliyoundwa na Prof. Lipumba.

Ally aliiomba mahakama itamke kuwa, ni ipi bodi halali kwa mujibu wa sheria za nchi na Katiba ya CUF 1992 toleo la mwaka 2014. Hata hivyo, baada ya kusikiliza pande zote mbili Jaji Masoud alifuta bodi hiyo.

Chama hicho cha upinzani cha tatu kwa ukubwa Tanzania Bara na cha pili kwa Tanzania Visiwani, kilitumbukia kwenye mgogoro mkubwa mwaka juzi baada ya Prof. Lipumba kujiuzulu na kisha kutaka kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti.

Kambaya akifafanua zaidi amesema, kuwa na Bodi ya Udhamini ndio msingi wa chama kuendelea kupata ruzuku na kwamba, bodi ndio wamiliki wa akaunti ya chama.

 Hata hivyo amesema, uamuzi uliotolewa ni wa kisheria na kuwa, kinachofuata kwa sasa ni kufuata utaratibu ili kuwa na bosi iliyokidhi vigezo.

“Athari yake ni kwamba, usipokua na bodi na hasa kwenye chama chenye kupata ruzuku ya serikali athari yake hamtaweza kupata ruzuku ya serikali.

“Ni kwa sababu sheria inahitaji bodi ya wadhamini ya chama kwa kuwa hao ndio wamiliki wa akaunti ya chama ambapo ruzuku ndio hupitishwa hapo,” amesema Kambaya.

Kambaya anayetajwa kuwa karibu zaidi na Prof. Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa amesema, ruzuku ni sehemu muhimu katika kuendesha chama ingawa vyama vya siasa vilianza kujiendesha bila kuwa na ruzuku.

Akizungumzia kutetereka kwa umoja ndani ya chama hicho Kambaya amesema, chama hicho hakijamfukuza mtu yoyote na kinachotakiwa ni kufuata Katiba ya CUF.

Amesema, umoja kwenye chama hicho hausimami kwa utashi wa mtu yoyote isipokuwa kuwa kufuata Katiba na taratibu iliyojiwekea chama ndio njia inayowezesha umoja huo kuimarika.

“Umoja kwa misingi ya Katiba sio kwa misingi ya utashi wa mtu. Katiba inaeleza misingi ya chama kwa hiyo yule anayehitaji kuendelea na shughuli za chama atafuata katiba ya chama,” amesema.

 Pamoja na kushindwa kwenye kesi ya Bodi ya Udhamini upande wa Prof. Lipumba, Kambaya amesema wanayo matumaini makubwa kuibuka na ushindi kwenye mashauri mbalimbali yaliyopo mahakamani

“Hoja itakuwa hiyo hiyo ya kisheria kwani sisi tunaamini tutashinda. Hata hili unaloliona sio upungufu wa Katiba ya CUF ni upungufu wa kutotekeleza sheria ya bodi ya wadhamini,” amesema.

Miongoni mwa kesi za chama hicho ni pamoja na ile namba 143 ya mwaka 2017 ya wabunge  wanane na madiwani wawili waliovuliwa uanachama  wao na Kambi ya Prof. Lipumba.

Pia kuna shauri namba 23 la mwaka 2016 la kuiomba mahakama kumzuia Prof. Lipumba kutofanya mkutano wowote mpaka shauri la msingi la mahakama itengue uhalali wa Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti wa chama hicho na kesi namba 248 ya mwaka 2018  ya kupinga chaguzi zozote ndani ya chama hicho.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

error: Content is protected !!