December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CUF kwazidi kufukuta, kufikishana kortini

Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

 

JUMUIYA ya Wanawake ya chama cha upinzani nchini Tanzania- Chama cha Wananchi (JUKECUF), imekiomba chama kuwafungulia kesi wanachama waliofukuzwa kwa madai ya kukikiibia chama hicho. Anaripoti Seleiman Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Hata hivyo, waliofukuzwa wamesema wao ndio watafungua kesi ili watoa tuhuma wathibitishe tuhuma zao.

Aidha, waliofukuzwa wamedai Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amezungukwa na genge la wapigaji.

Waliofutiwa uanachama CUF ni Ahmed Hamis, Mohamed Vuai, Ali Makame, Mtumwa Ambari, Hamida Huweshi, Dhifaa Mohamed Bakari, Chande Jidawi na Abdul Kambaya.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mtendaji wa JUKECUF, Anna Ryoba akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam huku kwa upande wa waliofukuzwa akizungumza Kambaya.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu 15 Novemba 2021

error: Content is protected !!