March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CUF kushirikiana na Ukawa uchaguzi madiwani

Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema (wakwanza)akiteta jambo na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimetangaza kushiriki uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata 43 hapa nchini unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, anaandika Faki Sosi.

CUF kimesema katika uchaguzi huo kitashirikiana na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kuunganisha nguvu za kisiasa.

Ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa ambavyo ni CUF, Chadema , NCCR-Mageuzi , na NRD.
Uchaguzi huo ni matokeo unafanyika kutokana na sababu zikiwamo wa vifo vya madiwani, kujiuzuru ama kuhama vyama na hivyo nafasi zao kubaki wazi.

CUF kimeweka mkakati wa kushiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Ukawa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Mbalala Maharagande, ambapo ameleeza kuwa Chama hicho kimepanga kutoa tamko rasimi juu makubaliano ya Ukawa juu uchaguzi huo Tarehe 8 hadi 11 Oktoba mwaka huu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Oktoba 4 mwaka huu ilitangaza kufanyika uchaguzi huo mdogo katika kata mbalimbali chini.

error: Content is protected !!