May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF kumkabidhi Rais Samia ilani zake

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari -CUF

Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kitamkabidhi ilani za chama hicho kuanzia Uchaguzi Mkuu wa 1995 hadi 2020 pindi ombo lao la kukutana naye litakapotekelezwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ombi hilo limetolewa na Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari CUF wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kuhusu siku 100 za Rais Samia madarakani.

“Tunamuomba afungue milango ya mashauriano na viongozi wa vyama, awe tayari kupokea ilani za uchaguzi mfululizo za CUF.  Tangu tumeanza mfumo wa vyama vingi, yapo mengi atajifunza na kumfanya awe rais wa mfano,” amesema Ngulangwa.

Rais Samia aliyeingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi mwaka huu.

Kiongozi huyo wa awamu ya sita wa Tanzania, anafikisha siku 100 keso tarehe 27 Juni 2021.

error: Content is protected !!