September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CUF kuanza ziara ya kushukuru

Spread the love

CHAMA cha Wananachi (CUF) kimesema kinatarajia kujaza mapengo ya nafasi za uongozi miezi miwili ijayo ili kukiimarisha chama pamoja na kurudi kwa wananchi kutoa shukrani kutokana na mchango wao ulioleta mafanikio kwenye chama hicho,anaandika Regina Mkonde.

Taarifa iliyotolewa leo na chama hicho imesema kuwa CUF imepata mafanikio kutokana na kushikilia  halmashauri 6 na kupata wabunge kumi Bara wakati awali ilikuwa na wabunge 2 na kwamba idadi hiyo haijawahi fikiwa na chama hicho toka mfumo wa vyama vingi kuanza.   

Aidha, CUF kimesema kuwa baada ya uchaguzi na changamoto zake kuna mapengo mbalimbali ya uongozi kuanzia ngazi ya matawi, wilaya mpaka taifa kutokana na sababu tofauti tofauti na baadhi ya viongozi nafasi zao bado ziko wazi.

Na kwamba jukumu la chama hicho kwa sasa ni kujaza nafasi hizo na baadhi ya maeneo, vile vile mwezi wa nane mwaka huu chama kitaitisha mkutano mkuu Taifa kwa ajili ya kujaza nafasi ya mwenyekiti wa taifa baada ya aliyekuwepo kujiuzuru.

Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF amewaambia waandishi wa habari kuwa CUF itafanya ziara nchi nzima kwa lengo la kuzungumza kuhusiana na mambo mbalimbali ya nchi.

“Takwimu zinaonesha kuwa wananchi waliuchoka uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), hivyo kuungana kwa vyama vya upinzani kumesaidia wananchi kukidhi haja zao, hivyo hatuna budi kurudi na kuwashukuru,” amesema Mketo.

Mketo amesema kuwa, CUF kwa kushirikiana na Ukawa itahakikisha inaondoa dosari zilizotokea katika uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 25,2015 ili kuhakikisha majimbo iliyopoteza yanarudi mikononi mwao.

“Licha ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kushikilia viti vingi vya ubunge, kusingekuwepo na dosari katika umoja huo Ukawa ingeshikilia majimbo yote ya Jiji la Dar es Salaam,” amesema na kuongeza.

“ Kama tungeunganisha nguvu na kusingekuwepo na dosari, Ukawa ingebeba majimbo yote na kuiachia CCM moja tu, lakini dosari ndizo zilizosababisha Ukawa kukosa baadhi ya majimbo ambayo ilikuwa na uhakika wa kuyapata.”

 

error: Content is protected !!