Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF: Jaji Mutungi ndiye chanzo cha vurugu
Habari za SiasaTangulizi

CUF: Jaji Mutungi ndiye chanzo cha vurugu

Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa. Kulia ni Maalim Seif Sharrif Hamad. Kushoto ni Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

CHAMA cha Wananchi ‘CUF’ kimemshutumu Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuwa  ndiye chanzo cha vurugu zinazoendelea ndani ya chama cha hicho, anaandika Hamisi Mguta.

Ni baada ya kutoa tamko la kulaani vurugu zilizofanywa na walinzi wa Lipumba lenye kichwa cha habari “Msajili wa vyama vya siasa kulaani vurugu zilizotokea katika mkutano wa wanaosemekana kuwa ni viongozi wa CUF na waandishi wa habari.”

Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, amesema pamoja na tamko hilo kuonesha Jaji Mutungi amesikitishwa na tukio hilo na kujitokeza kutaka wanachama wazingatie Sheria za Nchi na kulinda tunu za Taifa na amani, bado hana usafi wowote.

“Kwa bahati mbaya Jaji Mutungi ndiye chanzo cha vurugu zinazoendelea ndani ya CUF, hana usafi wa Maadili (Moral Authority and Moral Excellence) wa kujitokeza hadharani kulaani kitendo ambacho kimeasisiwa na mikono yake,” amesema Bimani.

Amesema, historia inaonesha kuwa machafuko makubwa yaliyotokea sehemu mbalimbali duniani yamesababishwa na mfano wa maamuzi ya hovyo kama haya ya Jaji Mutungi.

“Jaji Mutungi akiwa ni sehemu ya Washtakiwa/walalamikiwa katika mashauri kadhaa yanayoendelea mahakamani ameendelea kutenda vitendo vya hovyo na hata kudharau maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam katika shauri la madai Na.6 la mwaka 2003 baina ya Emmanuel Nyenyemela and Another Versus Registrar of Political Parties and Others’ lililokuwepo mbele ya Mheshimiwa Jaji Mihayo,” amesema.

Amesemaa Mahakama ilimuonya Msajili na Ofisi yake kwamba haina mamlaka ya kuingilia utendaji wa shughuli za ndani ya vyama kwa kubariki au kupinga maamuzi ya vikao vya chama husika. ilieleza kama ifuatavyo kwenye ukurasa wa pili wa hukumu:  “…The reliefs sought in this matter do not fall under section 20 of the Political Parties Act. They cannot therefore be sought by way of judicial review. In the same vein, I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make”. 

Tunapenda Msajili Mutungi atambue kuwa uamuzi na muongozo huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania haukuwahi kutenguliwa na mahakama yoyote ile na hivyo tunaamini kuwa Jaji Mutungi akiwa ni sehemu ya majaji ambaye hajastaafu wakati wowote anaweza kufanya kazi ndani ya Mahakama Kuu yeyote Tanzania akipangiwa kufanya hivyo, hatukutarajia ajiondoe ufahamu kiasi hiki katika uweledi wa taaluma ya sheria na kuhujumu muhimili ambao yeye ni sehemu.

“Jaji Mutungi amemuandikia Mkuu wa Jeshi La Polisi –IGP ampe ushirikiano wa kila hali Prof. Lipumba kila inapohitajika na asikilizwe kwa kila anacholielekeza jeshi hilo. Ushahidi wa hili kwa yanayoendelea hauhitaji tochi, ameziandikia benki mbalimbali nchini ikiwemo benki ya NMB Tawi la Ilala imfungulie akaunti yenye jina la CUF itakayosimamiwa na Prof. Lipumba ili aweze kumuingizia fedha za ruzuku ya chama,

“Ilipobainika njama hiyo na kuzuiliwa, sote tunajua nini kilijitokeza January 5, 2017 kwa kiasi cha Tshs 369 milioni kuingizwa katika akaunti ya wilaya ya Temeke tawi la benki ya NMB na baadae fedha zote kuingizwa kwa akaunti ya mtu binafsi Masoud Muhina, kutolewa zote siku moja na kwa kutumia mifuko ya rambo na mabegi zikapelekwa nyumbani kwa Prof. Lipumba,” amesema.

Amesema kuwa Jaji Mutungi ndiye aliyesababisha na mlezi wa vitendo vya kihalifu vinavyoendelea ikiwemo uvamizi wa Afisi Kuu ya Chama Buguruni Dar es Salaam, Tarehe 24/9/2016, uvamizi na kuvunja ofisi za Chama katika wilaya mbalimbali hapa nchini kunakofanywa na Prof. Lipumba na genge lake, uzuiwaji wa kufanyika kwa vikao halali vya chama kwa viongozi wa CUF Taifa na wabunge wa CUF maeneo mbalimbali kwa lengo la kumlinda Prof. Lipumba na kusudio la kutaka kukigawa chama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!