September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CUF, CCM wabanana Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeutaka upande wa mlalamikaji kupelekea fomu namba (21 b) katika kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na Idd Azan, aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni (CCM) dhidi ya Maulidi Mtulia, Mbunge wa Kinondoni (CUF), anaandika Faki Sosi.

Mlalamikaji katika kesi hiyo ni Azani ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kabla ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana dhidi ya Mtulia, mbunge wa sasa wa jimbo hilo.

Jaji Chochi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ndiye aliyesikiliza kesi hiyo leo katika Mahakama ya Kisutu amesema kuwa, upande wa mlalamikaji ufike mahakamani kesho na fomu hiyo ambayo ndio kiini cha kesi hiyo.

Jaji Chochi amesema kuwa, ingewezekana kuwaamuru waende kuchukua fomu hiyo nyumbani kwake lakini anahofia kuchelewa kutokana na Jiji la Dar es Salaam kuwa na foleni hivyo watachelewa.

Hata hivyo, Abubakari Juma, wakili wa upande wa mlalamikaji alipozungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama amesema kuwa, mahakama inataka kura za matokea ya uchaguzi zihisabiwe baada ya kuona kuwa fomu namba 21 b hazilingani “kutofautiana kwa fomu hizo kati ya kwetu na yake kutatoa tafsiri ya kuwa kuna hujuma.”

Nassor Juma, Wakili wa Upande wa Utetezi amesema kuwa, mahakama imegundua kuwa Azan anataka kuilazimisha ihesabu kura na kwamba, ndio maana leo kesi imeghalishwa kusilizwa mpaka kesho ili waje na fomu ya matokeo ya ubunge.

error: Content is protected !!